Sheria za barabarani

papercayenne

New Member
Joined
Jul 8, 2016
Posts
3
Reaction score
1
Naomba kufahamu dereva anapoishiwa petrol katikati ya Barabara ni kosa? Kama ni kosa kuna faini anatakiwa alipe au anapelekwa mahakamani?

Kuna ndugu yangu aliishiwa mafuta barabarani traffic police alipofika akaleta breakdown ikachukuwa gari na kulipeleka Tegeta Police station na kumuweka dereva mahabusu.

Naomba mwenye kufahamu anisaidie majibu ili hali hii isiwakute na madereva wengine.
 
mie ninavyojua angelipia tu gharama za hiyo breakdown iliyomtoa hapo katikati ya barabara
 
nchi ya matamko hii bwana,ukiingia barabara ya mwendokasi ng,oa matairi.
 
nilisikia walitangaza hata gariikiharibika njiani unalipa fine ......
 
Nionavyo mimi gari likiharibika na kama kuna uwezo wa kulisogeza pembeni ni bora kufanya hivyo. La sivyo weka ile triangle kuashiria hilo gari lina matatizo. Sasa utakuta baadhi ya watu gari linamatatizo, limeziba barabara au linasababisha wengine kupita kwa shida wakati kuna nafasi ya kulipeleka kando hata kwa kusukuma. Na kama kulikuwa hakuna uwezo/nafasi ya kulipeleka kando ya barabara je aliweka viashiria ya kuwa hilo gari lina matatizo (triagle)? si unajua kutokuwa na triangles ni kosa?
 
Dereva mzuri hawezi kuondoka na gari pasipo uhakika wa mafuta,upepo kwa tail na maji kwa rejeta,ikiyokea bahati mbaya na huna vi triangle weka hata majani mita kadhaa nyuma na mbele ya gari kuwajulisha wengine nje ya hapo ni uzembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…