Sheria za Askari wa usalama barabarani ziangaliwe upya ili kuondoa malalamiko ya Madereva kunyanyaswa na Askari.Leo katika taarifa ya habari ITV tumeona madereva kusitisha huduma za usafirishaji katika Mkoa wa Songwe kwa madai ya kunyanyaswa na askari wa barabarani.Hivi kama unagombea shamba na hakimu wa mahakama na ukapeleka kesi mahakamani na ukakuta unaegombea nae shamba ndie amekaa katija kiti cha kutoa haki je utapata haki? Iweje kwa askari wa barabarani wawe wanakamata dereva anaetuhumiwa anamakosa alafu askari huyohuyo anamamlaka ya kumhukumu dereva bila ya kuthibitishwa na mamlaka nyingine ,mimi naona kunahaja ya askari kuwa na kazi ya kukamata dereua na mamlaka nyingine ithibitishe kosa la dereva ndio adhabu itolewe kinyume na hapo haki ya madereva haitapatikana na rushwa barabarani haitaisha.Tunaomba ndugu zetu wa TLS waliangalie jambo hili na waishauri Serikali kwani jambo hili ni kero kwa Jamii ya Tanzania.