Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa itashauri iundwe sheria ya kuhasi wanaume wanaobainika kurudia matendo ya ubakaji na ulawiti mara baada ya kupewa adhabu ya kifungo cha miaka thelathini.
Ummy Mwalimu - Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Hayo yameelezwa leo mjini Dodoma na waziri wa wizara hiyo Mh.Ummy Mwalimu wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika itakayofikia kilele chake kesho juni 16.
Mh. Mwalimu amewataka wazazi wasiruhusu watoto wao kulala na watu wasiokuwa wazazi wao na hawafahamiki vyema hasa ndugu kwani wameendelea kuwa chanzo cha kuwaharibu watoto kwa kuwabaka na kuwalawiti.
Aidha Mh. Ummy amesema kuwa wizara yake pamoja na ile ya katiba na sheria imekwishampelekea mwanasheria mkuu wa serikali barua ya kutaka sheria ya ndoa ya mwaka 1971 irekebishwe kwani inashawishi watoto kuolewa wakiwa wangali watoto.
Chanzo: EATV