SHERIA, KANUNI, TARATIBU

Msengi Kiula

Senior Member
Jan 10, 2008
167
63
Tulikuwa kwenye mchakato wa Sheria mama-Katiba-; mabilioni yakatumika. Ikafika mahala- ika/mekwama.
Utawala mpya ukaanza. (Ma)waziri na Mkulu
_siyo kipaumbele
_sikuzungumzia wakati natafuta Kura
_tutaanza tena pale tulipoishia....nk nk.
Hili nalo litatatuliwa tu, tupende tusipende!

Sheria zetu kwenye Katiba hii hii tunayoiona ina mapungufu inaruhusu Rais kuteua wabunge 10. Nini kimetokea. Kuna mahala Mkulu ,pamoja na kuwa na washauri wabobezi, aliteleza. Kelele za "gender" zimefanikisha:
-Kijana wetu mahiri kwenda Berlin, angalau cha kuombea maji --Sehr geehrt .... Meine Damen und Herren- yaani ...Waheshimiwa ... Mabibi na Mabwana...,atatuwakilisha vizuri.
-Imemrudisha mama Kilango
-Imetoa fursa Mama Kikwete kuwa Mbunge.

Vita ya madawa ya kulevya ni nzuri. Hakuna anayeipinga. Tatizo ni inapopiganwa kwa hila.
Nini kimetokea?
-Kumbe kulikuwa na Sheria
Mkulu amekuwa muwazi amesema alikuwa haijui. Baada ya ushauri, ameteua mhusika na Waziri Mkuu pamoja na Mawaziri kadhaa wamepewa majukumu.
- Swala hili, limefukua mambo kadhaa ya kimaadili ,kijinai, kiweledi, na kimaamuzi.
Kila kipengele kinajitegemea.

Uteuzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki ni muhimu.
Hapa pana mjadala wa vifungu vidogo hiki na kile. Tumeshupalia kweli! Sawa.

Hebu tutafakari namna ya kuifanya nchi yeti kuwa ya viwanda
 
Back
Top Bottom