sheria bwelele, watekelezaji wapi sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

sheria bwelele, watekelezaji wapi sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Dec 22, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Unafika kwenye duka pekee linalouza petrol mjini(yapo mengi ambayo yamefungwa kwa sababu bei imeshushwa) unakuta msululu mrefu mithili ya nyoka. Kwa mbele karibia na pumpu unaona wawili wakizichapa kavukavu, unafuatilia unaambiwa wanapigana kwa sababu mmoja aliomba kwa mhusika auziwe nje ya utaratibu Wa mlolongo (queue discipline) ili aweze kumuwahisha mkewe hospitali, waliomtangulia wanaamua kumpa kipigo.

  Unatafakari na kujiuliza je ni kweli anayestahili kichapo hapo ni huyu anajayeribu kuokoa maisha ya mpendwa wake?

  Unashitushwa na tangazo kwenye redio yako kutoka kwa waziri anayelalama kuwa hajaona mtu anafungwa kuvunja sheria ambayo kumbe ipo inazuia hujuma kwa kuacha kuuza petrol, unashangaa zaidi kwa jinsi waziri mwenye mamlaka na mshauri wa rais anavyoonekana hana uwezo wa kulishugulikia tatizo hilo.

  Sasa unajridhisha kuwa wanaostahili kichapo ni hawa wanaoshindwa kutekeleza sheria walizoaminiwa kuzisimamia pamoja na wafanyabiashara wachoyo wanaopandisha bei haraka haraka inapopandishwa lakini wanaificha inaposhushwa.
  Unatamani uwaelimishe waungane kuwapelekea kichapo wahusika badala ya kupigana wao wasiokuwa na hatio
   
Loading...