Sharubati ya Kijenge.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,209
4,406
SHARUBATI YA KIJENGE. 1)Ulinywa bila kujua,ama kale kamzimu. Kamenza kujifufua,na kutoa chozi ndimu. Nawe bila jitambua,umesha kuvishwa njumu. Sharubati ya kijenge,yakutoa kwa kilinge. 2)ulijifanya kujua,leo imekulazimu. Aibu wajiumbua,hivi unaumwa pumu ? Vipi uliiendea,wakati siyo muhimu. Sharubati ya kijenge,kumbe nawe waipiga. 3)kumbe ilikunogea,hukuijua ni sumu. Ukaenda kuongea,na kile kitu adimu. Ona kimekuparia,amekutema mwalimu. Sharubati ya kijenge,nayo ina muda wake. 5)mengi uloyafichia,yametoka kule humu. Lile ulolibania,laanza kukulaumu. Natamani kukwambia,ile chai ni haramu. Sharubati ya kijenge,imekuvua kilemba. Shairi=SHARUBATI YA KIJENGE. Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha. +255625010160. iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom