GE2025 Shangwe Ayo: Uchaguzi wa 2025 ni mapambano ya kuikomboa Demokrasia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 hautakuwa wa kawaida bali utakuwa uwanja wa mapambano ya kuikomboa demokrasia ya Tanzania, ambayo kimeeleza kuwa imetekwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mwenezi wa ACT Wazalendo Taifa, Mheshimiwa Shangwe Ayo, wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Town School, kata ya Kambarage, Wilaya ya Shinyanga mkoa wa Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya Oparesheni Majimaji – kampeni ya kitaifa ya chama hicho ya kuhamasisha wananchi kulinda kura zao.

Shangwe amedai kuwa ushindi wa mara kwa mara wa CCM unatokana na matumizi ya hofu na mbinu zisizo za haki, akiwataka wananchi wa Shinyanga na Watanzania kwa ujumla kuwa na ujasiri wa kusimama dhidi ya vitisho hivyo.

Pia amegusia mwenendo wa chaguzi ndogo na mchakato wa uchaguzi mkuu ujao, akisisitiza umuhimu wa ushiriki wa wapiga kura kwa wingi na kuwalinda wagombea wanaotokana na wananchi wenyewe.

Your browser is not able to display this video.



Ziara hiyo ya Oparesheni Majimaji imekuwa ikifanyika katika mikoa mbalimbali nchini ikiwa na lengo la kuimarisha mtandao wa ulinzi wa kura, uhamasishaji wa kisiasa, na kuwapa wananchi mbinu za kikatiba na kisheria za kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi.
 
Tunasubiri hayo maigizo
 
Mimi mtazamo wangu Act na washirika wao akina Chaumwa Chaubwabwa wanashiriki kuizika japo zile chembechembe zake zilizosalia.Nawatakieni kila la kheri.
 
mbaf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…