SHAIRI: Wavulana Jilindeni na Mabinti Jichungeni

ONESMO MWAKAJILA

New Member
Jan 24, 2021
4
1
WAVULANA JILINDENI NA MABINTI JICHUNGENI

(Epsode 01)

Kijana aliyesoma miaka 17 kutoka shule ya msingi mpaka chuo kikuu bila kuwahi kutongoza mabinti, kuzini na mabinti wala kujichua aandika shairi ili kuwahamasisha vijana wengine kuwa inawezekana kujitunza katikati ya wengi walioharibika ili kutengeneza ndoa zao baadae zisizo na mawaa na hatia.

Acheni mahusiano
Hapo mnadanganyana
Huo siyo muungano
Bali mnachanganyana
Hizo hadithi za ngano
Yaani mnazugana
WAVULANA JILINDENI
NA MABINTI JICHUNGENI

Mimi hapa ni Jagina
Sijawahi lala na Binti
Sijawahi jamiana
Wala kunyonya matiti
Na Binti sijakutana
Wala sikuchimbi biti
WAVULANA JILINDENI
NA MABINTI JICHUNGENI

Mwenye sauti nyororo
Alikuja kunitega
Na Mwenye mwili mwororo
Ka asali ya masega
Likuja na mnyororo
Moyo ukapigapiga
WAVULANA JILINDENI
NA MABINTI JICHUNGENI

Na kope za kuvutia
Mrembo mzuri acha
Na nywele za bandia
Na za madukani kucha
Kitandani kunitia
Apate kunipekecha
WAVULANA JILINDENI
NA MABINTI JICHUNGENI

Niliukwepa mtego
Sikuweza kujinasa
Kwake Nei Wa Mitego
Sikuweza kumgusa
Ndipo nikaruka wigo
Kamwe sikumpapasa
WAVULANA JILINDENI
NA MABINTI JICHUNGENI

Mwili ni ulitetema
Nilipokumbuka ndoto
Nikawa nahemahema
Roho ikapata joto
Kashindwa kusemasema
Ndoto ikawasha moto
WAVULANA JILINDENI
NA MABINTI JICHUNGENI

Siyo kwamba nachekesha
Kwa kuyaandika haya
Kuna waliothibitisha
Wala sioni haya
Wengi wamehakikisha
Sichukulie vibaya
WAVULANA JILINDENI
NA MABINTI JICHUNGENI

0652260743

INJINIA____WA____YESU

FB_IMG_1682396802407.jpg


Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom