Shairi; Usinene ukamara

Shairi; Usinene ukamara

Galena

Member
Joined
Jan 4, 2016
Posts
9
Reaction score
15
1. Zituze zako fikara, sijelaumu ulimi
usinene ukamara, khifadhi zako kalami
sije kuoneka jura, Jahili uso harami.
Weka akiba maneno, usinene ukamara

2. Wengi mefikwa majanga, kwa kutohifadhi ndimi
Wakatukana wakunga, wakakufuru kwa semi
Nawe utalibenanga, hujazaa mwanamimi
Weka akiba maneno, usinene ukamara

3. Hako ajuae mwisho, si wewe wala si mimi
Sema fikiria kesho, sikughiribu ulimi
Kageuka kichekesho, ikakughura kaumi
Weka akiba maneno, usinene ukamara
 
1. Zituze zako fikara, sijelaumu ulimi
usinene ukamara, khifadhi zako kalami
sije kuoneka jura, Jahili uso harami.
Weka akiba maneno, usinene ukamara

2. Wengi mefikwa majanga, kwa kutohifadhi ndimi
Wakatukana wakunga, wakakufuru kwa semi
Nawe utalibenanga, hujazaa mwanamimi
Weka akiba maneno, usinene ukamara

3. Hako ajuae mwisho, si wewe wala si mimi
Sema fikiria kesho, sikughiribu ulimi
Kageuka kichekesho, ikakughura kaumi
Weka akiba maneno, usinene ukamara
Shairi la Mkinga
 
Back
Top Bottom