stable hech
Member
- Aug 4, 2015
- 20
- 6
umbo alokupa Mungu, silifanyie mchezo
lisikizie uchungu, usilitie uozo
sijitandie ukungu, kwa Mungu tapata tuzo
shukurani zipeane, kwa kuzawadiwa umbo
-----------------------------------
nyonga nzuri umepewa, nayo sura kadhalika
kwa wengine we ni dawa, tiba ilo uhakika
mtihani umepewa, umbo lako kutumika
shukurani zipeane, kwa kuzawadiwa umbo
------------------------------------
shukurani zipeane, Mola kuzawadi umbo
simuudhi hata tone, kuyepuka yake fimbo
upole uonekane, kwa Mola uwe hujambo
shukurani zipeane, kwa kuzawadiwa umbo
-----------------------------------
sijione malkia, kupatiwa umbo zuri
utakuja kuumia, siku yako kwa kaburi
tabaki kujichukia, ukikosa hiyo heri
shukurani zipeane, kwa kuzawadiwa umbo
--------------------------------------
kifo chako kikifika, umbo halitamaniki
wataenda kukuzika, wakuage marafiki
wote waliokusaka, wajua sasa huliki
shukurani zipeane, kwa kuzawadiwa umbo
------------------------------------
umbo lako liheshimu, lipatie na adabu
silifanye Kama simu, kukosa staarabu
simkosee Rahimu, ila kwake wewe tubu
shukurani zipeane, kwa kuzawadiwa umbo
Utunzi wa
©Stable Hech
{Mshipa wa damu }
lisikizie uchungu, usilitie uozo
sijitandie ukungu, kwa Mungu tapata tuzo
shukurani zipeane, kwa kuzawadiwa umbo
-----------------------------------
nyonga nzuri umepewa, nayo sura kadhalika
kwa wengine we ni dawa, tiba ilo uhakika
mtihani umepewa, umbo lako kutumika
shukurani zipeane, kwa kuzawadiwa umbo
------------------------------------
shukurani zipeane, Mola kuzawadi umbo
simuudhi hata tone, kuyepuka yake fimbo
upole uonekane, kwa Mola uwe hujambo
shukurani zipeane, kwa kuzawadiwa umbo
-----------------------------------
sijione malkia, kupatiwa umbo zuri
utakuja kuumia, siku yako kwa kaburi
tabaki kujichukia, ukikosa hiyo heri
shukurani zipeane, kwa kuzawadiwa umbo
--------------------------------------
kifo chako kikifika, umbo halitamaniki
wataenda kukuzika, wakuage marafiki
wote waliokusaka, wajua sasa huliki
shukurani zipeane, kwa kuzawadiwa umbo
------------------------------------
umbo lako liheshimu, lipatie na adabu
silifanye Kama simu, kukosa staarabu
simkosee Rahimu, ila kwake wewe tubu
shukurani zipeane, kwa kuzawadiwa umbo
Utunzi wa
©Stable Hech
{Mshipa wa damu }