Shairi:nambari Tano

Shairi:nambari Tano

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
35,759
Reaction score
86,409
1.Tano umeishika,nchi umeitikisa
hoja na viroja,kote vyasikika
taji wamekupatia,sifa tumezisikia.

2.Tano tumekupatia,lkn hatukutegemea
machachali wenye hali,mzigo umetuelemea
nyuso zimevilia,kwa vilio vya pundamilia.

3.Nambari kila kona,yavuma bila koma
wimbo nimeusikia,moyoni umeniingia
pigo limeniingia,maumivu nimeyasikia
macho nakukodolea,abadani sikutalajia.

4.labda mbali wajionea,vipofu tutaponea
muda tutajionea,taratibu tutasogea
hukumu tutatolea,muda utakapowadia.

5.fisi wenye figisu,walambe kwa kisu
wadhifu usio timilifu,tutaukata kwa kisu
amilifu mtiifu,tutampaka kwa sufu
tena kwa ukunjufu,wa mioyo yenye utimilifu.

shairi by KENZY
 
Hongera sana ndugu sasa tunaruhusa ya kufanya uchambuzi wa fani na Maudhui?
 
hii ndio faida ya sanaa,kichwa kichwa hautaelewa ila kwa kufikiri tushaelewa kuwa tano ni jamaa fulani hivi.
 
Back
Top Bottom