Shairi la kijijini

Shairi la kijijini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
Kijijini
Kijijini nakupenda, kunamahindi nandizi,
Kunayo mengi matunda, kunde, dengu na mbaazi,

Kuna mtamu mlenda, namkumbuka Shangazi,

Mwenzenu ninakupneda, sana kijijini kwetu.


Jamani babu nabibi, kijijini wamepozi,

Jamani kuku wa bibi, na wale wa babu mbuzi,

Nataka kwenda kwa bibi, kula mihogo na ndizi,

Mwenzunu na kukumbuka, sana kijijini kwetu.


Ifikapo asubuhi, JOGO la babau huwika,

Watu shambani huwahi,ili jembe kulishika,

Ndege nao hufurahi, mitini hufurahika,

Mwenzunu na kukumbuka, sana kijijini kwetu.


Amewaumba billahi, wazuri waloumbika,

Na angani hufurahi, wavutia kwa hakika,

Na Maji nayo Wallahi, TUNGINI yazizimika,

Mwenzetu nakukumbuika, sana kijijini kwetu.


Almasi H. Shemdoe, "

Tunda la Matumaini",
Dar es Salaam, Tanzania.
 
Daaaaah... hili shairi kidogo linitoe machozi!
Limenikumbusha home ni kiroho mbaya!

Hasa ukiangalia mjini mambo ! Wakati mwingine nuksi tu! Ukigeuka huku waliberali. Huku vibaka! Mara machangu!

Mnnssssssss! We acha tu!
 
Back
Top Bottom