Ndugu yenu kibatari
Sitaki chenu kiburi
Mlinitupa duhuri
Kwa hiyo yenu ghururi
Na nyingi zenu shururi
Niliweza zisubiri
Nikawa kama kaburi
Wala hamnidhukuri
Mlikuwa mwafikiri
Kuwa mimi ni faqiri
Wapi wenu uhodari
Na ule ujemedari
Nawapeni tahadhari
Kosa msilikariri
Munitundike vizuri
Kwenye uzi wa hariri
Kibatari una nini
Wajisifuni mitaani
Lau kama si sheni
singelitajwa abadani
Myaka ile ya dahari,
Umeme ulipojiri,
Kwa a njia ya bahari,
Wengi mlitahayari,
Kila kona palititiri,
Mwanga ka' magari,
Bila ya kutafakari,
Kwa dharau na shari,
Tena kwa kiburi,
Mkanitupa kibatari,
Bila hata ya hiyari,
Nyuma nikajisitiri,