Shairi:Fumbo mfumbo!

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
30,289
69,586
1.kulia niliona jembe,kushoto nikaona sembe
nyundo iliyomuuwa kenge,taratibu imevishwa pembe
rombo kapigwa chembe,katulia akila sembe.

2.ujio wa ujio,umekuja bila kilio
ujio wa wajio,umekuja na kilio!
uji wanjano,unachoma kama sindano.

3.pweza kajikweza,wababe hamtamuweza
mkimweka kwenye meza,kiulaini atawapoteza
siri ipo chini ya meza,kama hamtaki kupotezwa.

4.nyasi anawalisha,namagamba anawavika
mkipita mnajikweza,kumbe amewaweza!
kama kifimbo cheza,wa kas anawacheza.

5.kipara cha mkwala,juani bila kung'ara
bora avae ndala,mkononi ashike mwara
kichwani unalo swala,zonje acha ulafa.

6.mtutu watutuma,hili jitu halina huruma
kama nyika wanavuma,watashindwaje tunduma?
hakuna hata shutuma,kimyaa kama fatuma.

7.halima nakupenda,wivu sio kutenda
ujumbe umesikia,kipara amekuachia
haikuwa yangu nia,ila ujumbe nimekupatia.
 
Back
Top Bottom