Sauti ya nyikani
Member
- Jan 24, 2015
- 29
- 20
JINA LAKO LITANIPA TB.
Mpango chupa za coka, umeleta sokomoko.
mpenzi nawe wataka, chupa yenye jina lako.
nimemaliza maduka, Kibaha mpaka Keko.
Mpenzi badili jina, nisije pata TB.
Nasasa nimeshafika, kiwandani Makondeko.
Makreti napachika, godauni ndo niliko.
Jinalako nalisaka, Nyaminzi mwana Shiriko.
Mpenzi badili jina, nisije pata TB.
Stooni patashika, vumbi lake ni kiboko.
nabanja kama nabweka, na tumaini haliko.
Basi jiite Rebeka, nilipate pumziko.
Mpenzi badili jina, nisije pata TB.
Sauti ya nyikani.