Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,606
Mfanyabiashara wa Mirerani, Joseph Mwakipesile maarufu Chusa ametajwa tena kortini akidaiwa ndiye aliyetoa maagizo ya kuuawa kwa mfanyabiashara mwenzake, Erasto Msuya.
Mbali na kutoa maagizo hayo, imedaiwa kuwa bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) iliyotumika kumuua mfanyabiashara huyo, ilikodishwa eneo la mpakani la Namanga kwa Sh4 milioni.
Chussa alikuwa miongoni mwa washtakiwa wa kesi hiyo katika hatua za awali, lakini mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP) kwa kutumia mamlaka yake, alimfutia mashtaka hayo Aprili 17, 2014.
Hayo yamo katika maelezo ya onyo ya kukiri kosa ya mshtakiwa wa kwanza, Sharifu Mohamed anayemiliki migodi mitatu kitalu B, yaliyosomwa mahakamani jana mbele ya Jaji Salma Maghimbi.
Maelezo hayo yalisomwa mahakamani na shahidi wa 27 wa mashtaka, inspekta Damian Chilumba baada ya Jaji Maghimbi kuyapokea kama kielelezo baada ya kutupa mapingamizi ya mawakili wa utetezi.
Mawakili hao walikuwa wakipinga kupokelewa kwa maelezo hayo, wakidai mshtakiwa hakuyatoa kwa hiari yake na yaliandikwa kabla ya kukamatwa, madai ambayo Jaji Maghimbi aliyatupilia mbali hiyo jana.
Katika maelezo hayo, mshtakiwa anadaiwa kueleza kuwa Chusa alimpa maagizo ya kumuua Msuya Julai alipomtembelea katika Hospitali ya Mlale iliyopo Babati alikolazwa chini ya ulinzi.
Mshtakiwa huyo anadai Chusa alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo chini ya ulinzi wa askari magereza, baada ya kuumwa baada ya kusomewa mashtaka ya mauaji huko Mirerani.
“Mwishoni mwa Julai 2013 nilimtembelea Chussa na akaniambia Sharifu naomba uniangalizie shughuli zangu za madini zisikwame na ikibidi kugharamia shughuli za uendeshaji,” ananukuliwa kwenye maelezo hayo na kuongeza:
“Wakati najiandaa kuondoka Chusa aliniomba nimsogelee ana jambo nyeti ambalo hatakiwi watu wengine wasikie.”
Akinukuu alichoambiwa, shahidi huyo alidai:
“Unajua mateso yote haya ninayoyapata yanatokana na Msuya. Msuya ndiye amehonga niunganishwe kwenye kesi ya mauaji wakati sikuhusika.
“Kwa sauti ya chini Chusa aliniambia unajua wewe ni rafiki yangu nisaidie kumuondoa duniani Msuya. Nilipigwa na butwaa. Kasema fanya ufanyavyo ndani ya siku chache Erasto Msuya afe.”
Mshtakiwa huyo katika maelezo hayo anadaiwa kumweleza Chussa kuwa asingeweza kumuua Msuya, kwa kuwa hana ugomvi naye na ni mfanyabiashara mwenzake, kauli iliyoonekana kumuudhi Chusa.
“Alibadilika na kuonyesha hasira akaniambia kama umeshindwa basi nikitoka nitafanya mwenyewe. Baada ya kutafakari nikaona nikimwacha afanye mwenyewe angeniua kwa sababu alishaniweka wazi.
“Siku nyingine nilienda kumtembelea aliniuliza tena na kuniambia, au rafiki yangu unataka kunisaliti? Nilimuuliza anataka nifanyeje hiyo kazi akasema niwe mfadhili wa kazi yote akitoka atanirudishia,” ananukuliwa.
Katika maelezo hayo, mshtakiwa anadaiwa kueleza kuwa Chusa alienda mbali na kumweleza kuwa kuna kijana anaitwa Mredii (Shaibu Jumanne, mshtakiwa wa pili) ametoka gerezani ashirikiane naye.
“Mimi na Mredii tulionana Mirerani nikamuuliza kama amepewa maelekezo yoyote na Chussa, akasema ni kweli ana maelekezo ya kutekeleza mpango mzima wa mauaji,”anadaiwa kueleza hivyo na kuongeza:
“Tuliondoka kwenda Babati na kuonana na Chussa, lengo la kwenda ni kutaka anithibitishie Mredii aliyemtuma kwangu ndiye huyo naye akathibitisha ndiye amemwagiza kutekeleza mauaji hayo.
“Mredii aliniambia ngoja atafute watu wa kazi anaowajua na ataleta gharama za kazi nzima. Baada ya siku mbili, Mredii alikuja Arusha na kuniambia tayari ameshapata mtu mmoja.
“Nilikwenda nikakutana nao na Mredii akanitambulisha huyo mtu mwingine kuwa ni Ally Majeshi (mshtakiwa wa saba). Ally Majeshi aliniambia kikosi kitahitaji kuwa na watu wanne.”
Katika maelezo hayo, mshtakiwa huyo anadaiwa kueleza kuwa Ally Majeshi ndiye aliyetoa wazo la kusajiliwa kwa laini mpya na kununua pikipiki mbili, baada ya hapo watafute silaha.
Kwa mujibu wa maelezo hayo, mshtakiwa huyo anadaiwa kueleza kuwa Ally Majeshi alifanya mawasiliano na watu wengine wawili na siku iliyofuata alikutana nao Shamoo Guest House.
“Siku iliyofuata tulikutana Shamoo Guest House (inayomilikiwa na Sharifu) ndipo nilitambulishwa kwa Sadik (Jabir- mshtakiwa wa sita) na Karim (Kihundwa- mshtakiwa wa tano).
“Walisema wanahitaji usafiri na nikawapa gari yangu aina ya Toyota Land Cruicer LX pamoja na dereva wangu Mussa (Mangu- mshtakiwa wa tatu) wakaenda Namanga kutafuta silaha,” anaeleza Sharifu katika maelezo hayo:
“Zilitengenezwa laini mpya sita na kununuliwa simu mpya sita zilizosajiliwa kwa jina la Adam Leani. Ally Mjeshi ndiye aligawa simu hizo. Zililetwa pikipiki King Lion nyeusi na Toyo nyekundu.
“Mredii, Sadick na dereva wangu ndiyo waliokwenda Namanga kwa ajili ya kukodi silaha, lakini siku hiyo haikupatikana ilibidi walale. Siku iliyofuata niliwapelekea Sh4 milioni za kukodi silaha.
“Siku hiyo walileta SMG na ilipelekwa nyumbani kwangu nikaihifadhi hadi siku ya tukio. Siku moja kabla ya tukio yaani Agosti 6, tulikutana wote Shamoo Guest House kukamilisha mipango.
“Siku hiyo tulikubaliana tutumie mbinu ya kufanya biashara ya madini ili kumvuta marehemu. Ally Majeshi aliniambia nitoe jiwe moja (la Tanzanite) ili aende kufanya biashara na Erasto.
“Jioni alikwenda na jiwe lile wakakubaliana kufanya biashara siku inayofuata (tarehe 7.8.2013 siku ya mauaji) maeneo ya Bomang’ombe. Alimwambia lile jiwe wako wawili na mdogo wake”.
Katika maelezo hayo, mshtakiwa anadaiwa kueleza kuwa siku ya mauaji, pikipiki aina ya King Lion nyeusi iliwabeba Mredii na Sadick wakati aina ya Toyo ilimbeba Karim na Majeshi.
“Majeshi alishukia eneo la KIA (makutano ya barabara). Mimi nilikuwa na Suzuki na nilibaki na Jalila (Jalila Zuberi -mshtakiwa wa nne), ila hakutumika sana. Waliogopa kama wangemwacha angetoa siri.
“Mimi (Sharifu) ndiye nilibeba silaha hiyo kuelekea hadi Kia lakini tulipofika eneo la King’ori nilikabidhi silaha ile kwa Sadik aliyekuwa anatumia Toyo (pikipiki) nyekundu.
“Niliwaambia watakapomaliza kazi ya mauaji wasichukue chochote kwani hayo ndiyo yalikuwa maelekezo ya Chussa. Kaburu alinipigia simu baadaye na kuniambia kazi ya mauaji imekamilika.
“Kaburu ndiye mtu wa karibu na Chussa na ndiye alikuwa akimhudumia wakati akiwa amelazwa kule Babati, kuna wakati alikuwa akilala naye na alikuwa akijua mpango mzima wa mauaji.”
Mshtakiwa katika maelezo hayo ananukuliwa akieleza kuwa Kaburu ndiye aliyekuwa akifuatilia kila hatua ya mipango ya mauaji na yeye (mshtakiwa) alikuwa akimpa taarifa ili naye ampe Chussa.
“Baada ya tukio la mauaji kukamilika tulikutana wachache. Tulikutana na Mredii na Sadick maeneo ya Hoteli ya City Link na tukajaliana kuhusu malipo yao na tathmini ya kazi nzima,” anadaiwa kueleza.
Mshtakiwa anadaiwa kueleza kuwa washtakiwa hao walitaka walipwe fedha zao zote, hivyo siku hiyo aliwalipa Sh10 milioni, lakini kabla ya siku hiyo alikuwa tayari amewapa malipo ya awali ya Sh6 milioni.
“Baadaye Mjeshi na Sadik walirudi wakataka niwapeleke Babati. Niliendesha gari kwenda Babati na tulifika saa 3:00 usiku,” mshtakiwa anadaiwa kueleza hayo katika maelezo yake hayo.
“Nilipofika Babati nikaenda moja kwa moja kwa Chussa (hospitalini alikokuwa amelazwa chini ya ulinzi ) na nikamweleza kukamilika kwa kazi ya kumuua Msuya na Chussa alifurahi sana.”
Katika maelezo hayo, mshtakiwa ananukuliwa kuandika uthibitisho wa maelezo hayo kwa mkono wake na kuweka saini na dole gumba, akisema ameyatoa kwa hiari yake na bila kushurutishwa.
Kupokelewa kwa maelezo hayo ya Sharifu kama kielelezo, kunafanya maelezo ya onyo ya kukiri kosa yaliyopokelewa kuwa matatu; ya Mangu na Majeshi nayo yalishapokelewa na Mahakama.
Mahojiano utetezi
Akihojiwa na mawakili wa utetezi Majura Magafu na John Lundu kuwa kama wanayaamini maelezo hayo ya Sharifu kwanini Chussa na Kaburu siyo miongoni mwa washtakiwa, shahidi huyo alidai jukumu lake lilikuwa ni upelelezi.
Shahidi huyo alifafanua kuwa anaamini maelezo hayo ni sahihi ndiyo maana washtakiwa walikamatwa na kwamba suala la nani ashtakiwe na nani ni la DPP, hivyo ofisi hiyo ndiyo inapaswa kuulizwa.
Hata hivyo, alidai Sharifu na Kaburu walipokamatwa na polisi na kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo walikanusha kuhusika na akaeleza kuwa kutoshtakiwa kwao kortini hakufanyi maelezo ya Sharifu ya kukiri kosa yasiwe sahihi.
Ushahidi wafungwa
Baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake, wakili wa Serikali mwandamizi, Abdallah Chavulla alieleza Jamhuri inafunga rasmi kesi yao, kauli ambayo sasa inafanya upande wa mashtaka kufunga na mashahidi 27 badala ya 50 waliotajwa wakati inaanza 2015.
Jaji Maghimbi anayesikiliza kesi hiyo, alisema kwa kuwa amesikiliza kesi hiyo kwa miaka mitatu, atatoa uamuzi wa kama washtakiwa wana kesi ya kujibu au la Mei 14 baada ya kupitia ushahidi wote na vielelezo vilivyowasilishwa.