Ntate Mogolo
JF-Expert Member
- Jun 5, 2016
- 410
- 705
Lahaula! Maisha ya kitaa, vijiweni toka asubuhi sasa baaaasi! Ni wakati wetu sasa, wenye CV za ukweli, ambao kwa miaka mingi tumekuwa wahanga wa kukosa ajira kujitanua kwa mshahara kila mwezi na posho mbalimbali za safari nk.
Wenye vyeti feki walitudharau na kututambia sana. Jamii ilituona kama vile sisi ndo vilaza tulioshindwa shule, kumbe kinyume chake.
Serikali kupitia wizara husika, tangazeni sasa hizo ajira zilizoachwa wazi na hao wahalifu wa kughushi nyaraka. Ili na sisi tuweze kuanza kutupia makaratasi yetu ambayo ni halali.
Nadhani sasa tutaheshimiana kitaa! Madharau yao yamefika mwisho! KUFA KUFAANA Wahenga walinena!