Serikali za mitaa si jambo la Muungano!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,387
38,657
Wale wanaong'ang'ania Wabunge wa Viti maalum Zanzibar kupiga Kura kwenye Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam wajue kwamba suala la Serikali za mitaa si suala la Muungano. Na ndiyo maana haitawezekana kwa Wabunge hao toka nchi nyingine Kupiga kura kwenye uchaguzi wa serkali za mitaa wa nchi nyingine!!
 
Hata lingekuwa jambo la muungano sioni mantiki hata diwani wa kibaha kuja kupiga kura dar. Chama cha Mafigisufigusi kinalazimisha tu na cha ajabu hakuna wakusema hapa tumekosea-wao wanaona sawa tu. Huko tuendako giza lita tanda.
 
Ndiyo watu walitaka kutuaminisha kwamba kwa kuchaguliwa kwa Magufuli basi CCM itabadilika. Msingi mkuu wa CCM ni kutawala hata kama ridhaa ya kuendelea kuwapo madarakani haipo!!
Kwa kununuliwa na Lowassa mlitegemea kubadilika!!?
Leteni hoja za maana hapa

Naona mna tapatapa Hoja ya Zanzibar imebuma
Sasa mnaji Tutumua
 
Suala la umeya dsm hivi magufuli na majaliwa wanafurahia

Tena serikali za mitaa ni lipo chini ya Waziri Nkuu, Majaliwa na kila siku anaaita wanahabari na kutuambia Rais kamwagiza aende bandarini, ........ kamwagiza mawaziri ambao hawajajaza form hadi sa 12 wawe wamerudisha vinginevyo watakuwa wamejifuta kazi nk nk. Kwa nini hajamwagiza asimamie uchaguzi wa Umeya ambao upo chini yake!!!???
 
MBONA NI WAZI KABISA KUWA UMEYA WA DAR HAUCHAKACHULIKI!
CCM kuchakachua si lazima washinde, hata wakishindwa watachakachua tu, hivi unadhani wanashindwa kuiweka Halmashauri ya jiji ya Dar es salaam chini ya Uangalizi wa TAMISEMI? Huo si utakuwa ni uchakachuaji?
 
CCM kuchakachua si lazima washinde, hata wakishindwa watachakachua tu, hivi unadhani wanashindwa kuiweka Halmashauri ya jiji ya Dar es salaam chini ya Uangalizi wa TAMISEMI? Huo si utakuwa ni uchakachuaji?

NAKUBALIANA SANA, LAKINI NAKUMBUKA LIWAYA MOJA YA TAMTHILIYA YA O LEVEL MIAKA ILE. "TAMBUENI HAKI ZETU", WALITUFUNDISHA WAO NA WANADHANI TUMESAHAU. ILISISITIZA, "HAKI YA MTU HAIPOTEI, HUCHELEWESHWA TU" (HASA MNYONGE)
 
Back
Top Bottom