Nimejumuisha afrika nzima ila nitaeleza kuhusu nchi yangu kwa machache kidogo.
Serikali yetu si msaada kwa mwananchi ukikurupuka kutafakari utakimbilia mengine kuona yanayofanyika kuletewa wewe mwananchi kama hospitali, shule na n.k
Ili ninalotaka kusema kuwa sio msaada kwa mwanchi limebeba neno moja "FURSA".
Tunapozungumzia fursa basi kwa tanzania fursa zipo nyingi ila kutokana na serikali yenyewe itaki uwe na fursa labda kwa chama hiki ambacho kishafanya fursa hii kutokuwepo watumie kama mtaji wakushinda chaguzi.
Tanzania tumebalikiwa kuwa ardhi kubwa yenye kulimika kila kitu, bahari, mito, nchi zilizotuzunguka kimaitaji na n.k.
Je ni kipi ambacho serikali kutokuwa msaada. Ni jambo linalosikitisha mtu kuwa na ardhi au mifugo alafu serikali ikashindwa kukunyanyua kuwa mkulima au mfugaji yule mwenye nyumba zuri, ghala zuri, mashine nzuri na masoko ya huahakika.
Ili jambo linaumiza sana pale viongozi wanapokwenda nchi za watu ambao wenye ardhi ni wachache ila serikali imeweka nguvu kuhakikisha mwenye ardhi kupata msaada mkubwa kwa kila jambo, leo usishangae mkulima mmoja anaweza kulisha wilaya moja mwaka mzima. wakati huku tukikazana na jembe na kupuliza dawa dumu liko mgongoni.
Serikali ni kipi inaogopa? Kutomuwezesha mwananchi mwisho wa siku asiogopwe.
Leo ukifika ulaya ukajitambulisha mbele za watu kuwa umetokea familia ya mkulima wanashtuka wanahisi ni mtu mkubwa kumbe mshika jembe na ikifika uchaguzi doti ya kanga.