.....Wanatudanganya bwana,unaweza kushangaa jinsi viongozi hawa wajinga wanavyo hubiri umaskini wa ardhi hii!sasa unashindwa kujua kama wamekamilika au ni ushamba tu wanataka bwawa ka kuogelea,gari automatic,deal ofisini,waitwe Mungu watu.
Angalia magari ya serikali ya TZ ni ya anasa sana,halafu hayapakii au kutoa msaada kwa mwananchi wa kawaida,yaani unaonekana gaidi au mchafu vile.
Huko vijini wananchi hawana huduma muhimu za afya,elimu,maji,chakula,nyumba,ardhi wanayomiliki kwa asili haina hati wala nini!
Hapo ndio unaposhangaa na kujiuliza vichwa kama ipo sawa sawa,ni kwa vipi unahubiri umoja wa kisiasa wa East Africa wakati sheria na sera zako za ardhi nk ni hovyo hivi?
Ardhi haiwezi kuwa mali ya umma ktk nchi ya kibepari/soko huria,hiyo ni danganya toto na pindi watz watakapojua nini mfumo wa soko huria hapata kalika maana kila moja atataka kumiliki ardhi na itakuwa haipo hapo sasa ndio mtajutia kutoa uraia kama peremende.
Watu wanaota kuwa daima Tanganyika itakuwa shamba la bibi!No ipo siku na sio nyingi haya yote yatatokea, kama hauamini angalia migogoro ya ardhi,watu wanavyonunua ardhi.
YAANI UJANJA WA KUEPUKA HAYA YOTE NI KUTOA HAKI KTK ARDHI.Pimeni ardhi yote ya vijijini na wenyewe wapewe hati ili watajirike.