Nchi yetu duniani inahesabiwa na kuchukuliwa kama kati ya nchi masikini duniani, ni ukweli usiopingika lakini mpaka sasa hivi serikali yetu imechukua hatua gani kutikomboa na umaskini huu?
Nchi ni maskini, sasa kuna ulazima wa maslahi ya nchi kutumika kulipa viongozi wa serikali hela nyingi? Kwani wao hawajui nchi ni maskini?
Kuna ulazima wa awao kuendesha magari ya kifahari wakaati wanajua nchi ni maskini? Uongozi ni wito lakini serikali imefanya uongozi ni kazi ndio maana wanarogana.
Serikali isitudangaye kwamba inafanya jitihada zozote kutuondoa kwenye umasikini kwa kutumia hicho hicho kidogo kilichopo kurahisisha maisha yao na familia zote wakisahau hata wawe na pesa nyingi hawatalala kwenye vitanda viwili kwa wakati mmoja.
Wanafunzi wamekosa mikopo, wazazi wao wanalipa kodi nyingi kila kukicha kwa ajili ya kununua mashangingi.Serikali ikubali tupite mapito magumu ili tufikie pazuri lakini kwa staili ya kutumia kidogo hichohicho kwa ajili ya starehe.