Serikali yazindua mfumo wa matibabu kwa mtandao

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1553782847353.png



SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo imezindua Mfumo mpya wa utoaji huduma za afya kwa njia ya mtandao utaosaidia kurahisisha utoaji wa huduma za Afya ikiwemo huduma za matibabu ya kibingwa kwa wananchi.

Uzinduzi huo umefanyika leo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 7 wa masuala ya Sayansi na Afya uliowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki kujadili kwa pamoja juu ya njia ya kufanikisha malengo ya Afya ya umoja wa mataifa.
Mhe. Samia alisema kuwa nchi za Afrika Mashariki zikijikita katika utoaji huduma kwa mfumo huo kwa ushirikiano wa pamoja, itakuwa ni njia sahihi kwa nchi hizo kufikia malengo ya milenia na huduma za afya kwa wote.

“Tunapaswa kufikia malengo tuliyojiwekea kama bara la Afrika na nchi za Afrika mashariki, mkutano huu si tu wa watafiti kutoka Afrika Mashariki bali ni muhimu kwa wadau wote katika sekta ya afya tufanye kazi kwa pamoja kukamilisha malengo haya,” alisema Mhe. Samia.

Mhe. Samia aliendelea kusema kuwa tiba mtandao itawezesha na kuongeza ufanisi katika kufanya uchunguzi, utoaji wa tiba na dawa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali, hivyo kurahisisha utoaji huduma za Afya kwa Wananchi.

Aidha, Mhe. Samia Aliongeza kuwa tiba mtandao itapunguza gharama za wagonjwa na wanaowahudumia kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za matibabu katika Vituo vyakutolea huduma na Hospitali.

Nae,Waziri wa Afya na mapambano dhidi ya VVU kutoka Burundi Dkt. Thaddee Ndikumana alisema programu hiyo itakuwa ikitumika kwa nchi za Afrika Mashariki itakuwa chachu katika kuleta Mapinduzi ya utoaji huduma za Afya kwa Wananchi wa Afrika Mashariki.

“wananchi wa Burundi watakuwa wanaweza kupatiwa matibabu na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa nchini kwao bila kuja Dar es Salaam hiyo ni kitu muhimu tutakuwa tunabadilishana uzoefu raia wa Burundi walikuwa wanakuja kila siku sasa safari zitapungua, watabaki Bunjumbura na huduma watapata.” Amesema Dkt. Thaddee Ndikumana

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa daktari atakuwa na uwezo wa kuwasiliana na madaktari wenzake katika mtandao na madaktari bingwa wa nchi nzima wanaona lile tatizo jambo litalosaidia katika kutoa huduma bora kwa Wananchi wan chi za Afrika Mashariki.
Waziri Ummy Mwalimu, aliendelea kusema kuwa tayari Tanzania ilishaingia katika mfumo wa matumizi ya kidijitali katika utoaji wa huduma kwenye maeneo mengi, na umekuwa na msaada mkubwa sana katika Sekta ya Afya.

“Nchini Tanzania miezi mitatu iliyopita madaktari walianzisha mfumo mawasiliano kupitia dijitali ambao unawawezesha madaktari bingwa kuwasiliana moja kwa moja na madaktari waliopo pembezoni na umeweza kuokoa maisha ya kinamama sita ambao walikuwa wanajifungua,” amesema Ummy.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Nimr Profesa Yunus Mgaya alisema kuwa mfumo huo utapunguza gharama za utoaji wa huduma za afya na itaongeza ufanisi katika utendaji wa kazi wa wahudumu wa afya.

“Italeta utaalamu wa hali ya juu wa kibingwa katika maeneo ambayo hauwezi kufikika kwa mfano wataalamu wanaweza kuwepo Muhimbili na mgonjwa akawa mbali ambako hapafikiki kirahisi na hiyo ni msaada mkubwa sana kwa kuwa hizi huduma kama ingetakiwa wataalamu wawepo kule gharama yake ingekuwa kubwa sana,” alisema Prof. Mgaya.

Nae, Waziri wa Mambo ya Nje, Palamagamba Kabudi amesema kuwa nchi ya Tanzania itanufaika zaidi katika mfumo huo katika kulifikia lengo namba tatu la malengo ya milenia, pia itasaidia kufanikisha lengo la afya kwa wote ifikapo 2030
 
Hili linawafikia hata wasio na bima ya afya?! Na tunaenda wapi tukitaka kupata huduma hii ya telemedicine?! Inapatikana kwa simu au ni webpage maalum?! Au kuna App maalum kwa ajili ya hii huduma?! Na je lazima niwe na internet au hata offline?!Je ipo muda gani asubuhi, mchana, usiku au masaa 24?! Mgonjwa anapohitaji vipimo inakuwaje?! Kuna electronic medical chart za kuhifadhi kumbukumbu za mgonjwa au wanazihifadhi vipi?!
Prescription za dawa napata kwa electronic pia au hii ni kwa basic consultation tu?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lazima kuuanzisha usajili kwanza wa mtu na simu yake na pawepo utaratibu wakukatwa kupitia simu ya mtu mojamoja ndiyo italeta ufanisi kwenye huu mfumo
 
Back
Top Bottom