Serikali yazifungia kampuni tatu za uwakala wa ajira

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Serikali yasitisha Shughuli za Kampuni Tatu (3) za Wakala binafsi wa huduma za ajira hapa nchini kutokana na kukiuka matakwa ya sheria ya huduma za ajira Na.9 ya mwaka 1999 na Kanuni zake.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi na wadau mbalimbali kuhusu utaratibu unaotumiwa na baadhi ya wakala binafsi wa huduma za ajira nchini.

Kampuni zilizofutiwa usajili baada ya kukiuka sheria ni pamoja na Sasy Solution Company Ltd, Bravo Job Centre Agency na Competitive Manpower International Ltd ambapo Kampuni hizo haziruhusiwi kujihusisha na shughuli za Uwakala binafsi wa ajira nchini.

Akifafanua Mhe. Mhagama amesema kuwa uchunguzi umebaini ukiukwaji wa taratibu za usajili ambapo baadhi ya mawakala wamekuwa wakitumia nyaraka zilizopatikana kwa njia isivyo halali katika kujipatia leseni za uwakala hali iliyowawezesha kukwepa kodi na kujipatia faida.

Aliongeza kuwa ukiukwaji wa taratibu za kisheria umeleta athari mbalimbali kwa wafanyakazi hasa kwa wale wanaoenda kufanya kazi Mataifa ya Nje ambapo wafanyakazi hao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ubaguzi na unyanyasaji katika ajira, malipo ya mishahara na stahiki mbalimbali.

Aidha, Mhe. Mhagama amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imesitisha mara moja shughuli za Mawakala Binafsi wa huduma za Ajira zinazohusika na kuwatafutia kazi wafanyakazi nje ya nchi (cross border placement) hadi hapo Serikali itakapoleta mfumo wa kusimamia jambo hili na kutoa taarifa kwa umma.

Chanzo: EATV
 
Kazi ipo kweli kweli ....

Kampuni inapataje nyaraka za serikali kwa ujanja!?

Una mfungiaje mtu bila kumuwajibisha aliye husika kutoa nyaraka na vibali feki kwa kampuni hizo!?
 
Ahsante
 
668344ba829a5f62ad5fa5b45e10dd72.jpg
si ndo hawa aisee na kina mtemvuu duhh
 
Madalali Wapo Kila Kona Kwenye Makampuni Na Wanaingiza Pesa Nyingi Huku Wakiwanyonya Wafanyakazi Sasa Nashangazwa Waziri Kayaona Hayo Tu Yanayodili Na Wafanyakazi Wa Nje Wakati Yahumu Humu Nchini Yamemshnda

we acha tu mkuu tunapoelekea huku
 
Kazi ipo kweli kweli ....

Kampuni inapataje nyaraka za serikali kwa ujanja!?

Una mfungiaje mtu bila kumuwajibisha aliye husika kutoa nyaraka na vibali feki kwa kampuni hizo!?
Unakata matawi unaacha shina na mizizi, mti lazima uendelee kukua tu.
 
Back
Top Bottom