Serikali yatoa majina ya waliochaguliwa kidato cha tano mwaka wa masomo 2016/2017

Naisoma360

JF-Expert Member
Jan 23, 2015
821
491
Ofisi ya Rais TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2016. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.

Jumla ya wanafunzi 65,720 wakiwemo wasichana 29,457 na wavulana 36,263 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 34,064 wakiwemo wasichana 13,466 na wavulana 20,598 sawa na asilimia 52 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 30,897 wakiwemo wasichana 15,445 na wavulana 15,452 sawa na asilimia 47 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara na wanafunzi 759 wakiwemo wasichana 220 na wavulana 539 sawa na asilimia 1 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ufundi.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2016 wataanza muhula wa kwanza tarehe 11 Julai, 2016 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 24 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi mwaka 2016 pamoja na fomu za kujiunga (joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz

Imetolewa na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI

Tumia link hii kupata matokeo Waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi 2016
 
So unataka kusema kwamba kutokana na kucheleweshwa kwa post hawawezi kuongeza muda wa kuwasili#nijuze mkuu coz Nina ugeni na hili
 
wakuu niangalizieni mpwa wangu ibrahim b aweso s.4573\105 uwanja wa taifa secondary
 
Wameyatoa katika mtindo ambao haueleweki coz majina kama vile hayapo yote
 
Hii nchi hata ukitafuta tatizo ni nini hujui uanzie wapi. Kutoka leo hii hadi tar 11 ni kama wiki mbili tu sasa hayo maandalizi yatakuwa yamefanyika lini. Kwanini kila.kitu lazima kiwe ni chakushtukiza? agrrrryyyy.
 
Serikali imetangaza majina ya wanafunzi watakaojiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2016/2017.Wanafunzi waliochaguliwa ni 65720.Itaendelea kadr ya mahitaji........
 
Back
Top Bottom