kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,676
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashantu Kijaji.
Serikali imetakiwa kupunguza makato ya kodi kwa wafanyakazi wanaokatwa makato ya juu yanayofikia asilimia 30.
Rai hiyo ilitolewa bungeni mjini hapa jana na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Hawa Chakoma, wakati akiuliza swali la nyongeza, akitaka kujua kama serikali ina mpango wowote kwa wafanyakazi ambao wana makato makubwa ya kodi yanayo fikia asilimia 30.
Akijibu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Angelah Kairuki, alisema wizara yake imeshawalisha mapendekezo ya kupunguza kodi kwenye kamati ya kikosi kazi (Taxsiforce) kwa ajili ya kulijadili suala hilo.
Alisema kikosi kazi hicho hicho kinajumuisha Wizara ya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Katika swali la msingi, mbunge huyo alitaka kujua namna serikali ilivyojipanga kutekeleza jambo hilo muhimu kwa ustawi wa wafanyakazi.
Akijibu, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashantu Kijaji, alisema, mfumo wa kodi ya wafanyakazi uliopo sasa umeweka viwango kwa kuzingatia kipato cha mfanyakazi ambapo kiwango cha kodi hupanda kadri ya kipato cha mfanyakazi kinavyopanda.
CHANZO: NIPASHE