Serikali yasema Mara waongoza kuwa na walemavu wengi nchini

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni.Mkoa wa Mara kwa mujibu wa ofisi ya waziri mkuu inayoshughulikia walemavu unaongoza nchini kwa kuwa na walemavu wengi .Na walemavu hao wengi ni wale wanaotokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Mkoa wa Mara nasikia kila duka la dawa lina dawa ya vidonda.Dawa za vidonda ni dawa muhimu mkoa wa Mara kuliko dawa za malaria au panadol na mtu unatakiwa kuwa nayo akiba mfukoni popote unapokuwa ukiwa mkoani Mara.Sababu ukimbishia tu hata kondakta kwenye daladala kinachofuata waweza jikuta unahitaji bandeji au dawa ya kidonda haraka kushughulikia eneo uliloumia baada ya kondakta kufanya vitu vyake chap chap.

Mkuu wa mkoa wa Mara Magesa Mulongo kazi anayo kupunguza viwango vya walemavu wanaotokana na kupigana vichwa,mikuki,mapanga na marungu nk
 
Waongo bana mbona mimi naishi mkoa wa mara na si waoni walemavu wanaosemwa kwa wingi. Ni vema tuwe wakweli unless mtoa habari hii nae ni mlemavu anayewafahamu wenzake kwa idadi yao kulinganisha na mikoa mingine.
 
Hii ni kwa mujibu wa takwimu za walemavu ambazo zinapatikana pia ofisi ya takwimu taifa (NATIONAL BUREAU OF STATISTICS) sio vya kutunga.
 
Waongo bana mbona mimi naishi mkoa wa mara na si waoni walemavu wanaosemwa kwa wingi. Ni vema tuwe wakweli unless mtoa habari hii nae ni mlemavu anayewafahamu wenzake kwa idadi yao kulinganisha na mikoa mingine.
Yaezekana unaishi Mara, Musoma mjini.

Njoo huku Rung'abhure, Machochwe, Nyamng'orori, Mugumu, Rwang'enyi, Kitarang'anda, Gherenge n.k ndio utajua
 
Wale jamaa huwa hawana utani na ndiyo maana ccm haina nguvu sana huko

Angalia wabunge wa mkoa wa Mara,Eti CCM haina nguvu!!!! unaota.

1.Bunda -CDM (Ester Bulaya)
2. Musoma mjini -CCM (Vedastus Mathayo)
3. Musoma Vijijini -CCM (Prof. MUHONGO )
4. Butiama -CCM (Nimrod Mkono)
5. Bunda Vijijini - CCM (Boni)
6. Tarime Vijijini -CDM (John Heche)
7. Tarime Mjini -CDM( Ester Matiko).
8. Mwibara - CCM (Kangi Rugola).
9. Rorya - CCM (Lameck Airo)
 
watani zangu wametisha...
Kilema cha mapanga na sime ndio nyumbani...
Kuwa na kovu ni kama moja ya urembo pande zile
 
Angalia wabunge wa mkoa wa Mara,Eti CCM haina nguvu!!!! unaota.

1.Bunda -CDM (Ester Bulaya)
2. Musoma mjini -CCM (Vedastus Mathayo)
3. Musoma Vijijini -CCM (Prof. MUHONGO )
4. Butiama -CCM (Nimrod Mkono)
5. Bunda Vijijini - CCM (Boni)
6. Tarime Vijijini -CDM (John Heche)
7. Tarime Mjini -CDM( Ester Matiko).
8. Mwibara - CCM (Kangi Rugola).
9. Rorya - CCM (Lameck Airo)
Kangi lugola muomba rushwa naye unamuhesabia?
 
Back
Top Bottom