Serikali yaitisha uchaguzi Yanga

Sinkala

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
1,773
687
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeandikia barua klabu ya Yanga kuiagiza iwe imekwishafanya uchaguzi wake hadi kufika Aprili 15, mwaka huu. Yanga imekwishapokea barua hiyo kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT)

Yanga kwa sasa ipo chini ya uongozi ambao umekwishamaliza muda wake, uongozi ambao uliingia madarakani Julai 15, mwaka 2012 katika uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi za viongozi waliojiuzulu. Uongozi huu ulishamaliza muda wake mwaka 2014
 
Dawa ni kubadilisha tu mfumo wa kuziendesha timu zetu kwa kuwamilikisha matajiri waziendeshe kibiashara badala ya kuendelea kuukumbatia huu mfumo wa mwaka 47 wa kutegemea wanachama.

Azam fc ndani ya miaka michache tu imepiga hatua wakati Yanga fc na mtani wake tangu 1935 wamefanikiwa tu kumiliki mashabiki wengi zaidi ya hapo ni shida tupu.
 
So TFF Wameshindwa Kuilazimisha Yanga Kufanya Uchaguzi Kwa Miaka Yote 2!!!?? Mbona Waliweza Kuwalazimisha Toto Africa Na Coastal Union Kufanya Uchaguzi, Lkn Walishindwa Kufanya Hivyo Kwa YANGA!!?
 
So TFF Wameshindwa Kuilazimisha Yanga Kufanya Uchaguzi Kwa Miaka Yote 2!!!?? Mbona Waliweza Kuwalazimisha Toto Africa Na Coastal Union Kufanya Uchaguzi, Lkn Walishindwa Kufanya Hivyo Kwa YANGA!!?
Tena rais wa TFF Malinzi nilimsikia akitamka suala hili kulisimamia yeye mwenyewe, ni miezi mingi sasa tokea atamke hivo.
 
Back
Top Bottom