Serikali yaagiza kutiwa mbaroni wakala wa Pembejeo kwa tuhuma za rushwa Morogoro

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Serikali wilayani Ulanga mkoani Morogoro imeamuru kutiwa mbaroni kwa wakala wa usambazaji wa Pembejeo, Novatus Naningwa na wasaidizi wake pamoja na Afisa mtendaji wa kata ya Kichangani na wa kijiji cha Kichangani wilayani humo, wakituhumiwa kuwarubuni wananchi kuchukua fedha badala ya vocha za Pembejeo.

Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Christina Mndeme amekiri kufikia uamuzi huo, baada ya wakala huyo, wasaidizi wake na kiongozi wa kata ya Kichangani na kijiji cha Kichangani kubainika walikuwa wakiwarubuni wananchi kuchukua kiasi cha shilingi 5000 ili wasaini wamepokea vocha hizo za serikali ambazo nusu ya Gharama yake imekuwa ikilipiwa na Serikali.

Amesema wakala huyo alipewa dhamana ya kusambaza vocha hizo za Pembejeo katika kata tatu za Kichangani,Lupiro na Milola,lakini yeye na wasaidizi wake,Kuchungi Mussa, Ponsiasi Chanja,Christopher Ponela na Rashid Msasa, walishirikiana na mtendaji wa kata na wa kijiji na kuwarubuni wananchi Wachukue vocha,badala yake walisaini vocha Hizo na kupewa shilingi 5,000 kwa kila mmoja.

Hata hivyo Amesema baada ya Uongozi wa Wilaya kupata taarifa kutoka kwa raia Wema na Diwani walimuandikia wakala huyo barua ya kumsimamisha kuendelea na Huduma ingawa aliendelea na zoezi hilo hivyo kuamuru watuhumiwa hao watiwe mbaroni ili kufikishwa mahakamani,huku Mtendaji wa kata na mtendaji wa kijiji cha Kichangani wakikimbia na wanaendelea kutafutwa.
 
Kwenye pembejeo ndio kwenye matatizo
Kupeleka watu wengi kuona kilimo nikama dhahma fulani
 
Back
Top Bottom