A
Anonymous
Guest
Huku kwetu Kata ya Mbezi Msumi, Dar es Salaam viongozi wa Serikali za Mtaa wanatulipisha Shilingi 5,000 kila mwezi kwa ajili ya kuzoa na kukusanya takataka, kulipa sio ishu, ila wanakulazimisha ulipe uwe una taka au hauna hilo ni juu yako.
Mfano wanaenda hadi kwenye maduka ya jumla ambayo uchafu wao labda ni michanga tu ambayo inaingizwa ndani na wateja, nao wanalazimishwa walipe, usipolipa wanakuchukulia hatua.
Hilo ni cha mtoto, kubwa zaidi kuna jamaa yetu hapa ana duka alitozwa faini shilingi 30,000 kutokana na suala hilohilo la takataka, akalipa na akapewa risiti kabisa yam ashine, lakini walipoondoka tukai scan ile risiti kuona fedha inaelekea wapi, hatukupata jibu.
Risiti wanaolipisha watu mtaani kweli unaona zinatoka kwenye mashine yao lakini uki scan hauoni pesa inaelekea wapi, wakati ukichukua risiti ya mafuta kwenye kituo cha mafuta au sehemu nyingine wanapotoa risiti ya elektroniki unaona kabisa flow ya fedha yako inapoelekea.
Inavyoonesha kuna upigaji unafanyika hapo si bure, Mamlaka ziamke zifuatilie hizi mashine zinazotumiwa Kata ya Mbezi Msumi na kwingineko, inawezekana hii ni sample tu ya kinachofanyika sehemu mbalimbali.