Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Mambo yanayoendelea kwa sasa katika nchi yetu yanalazimisha watu kujiuliza kama serikali ya awamu ya tano ya Mh. Magufuli iko mbioni kusimamisha katika ya nchi kufanya kazi. Wananachi tunaanza kuona sheria za nchi zinakiukwa waziwazi katika kutekeleza shughuli za bunge, shughuli za seikali pamoja na taasisi zake ikiwemo polisi.
Utaratibu wa kusimamisha katiba ya nchi hufanyika hasa katika nchi ambazo mtu au kikindi cha watu wanapopindua nchi. Katika nchi ya kidemokrsia kama Tanzania ambayo inafuata mfume wa vyama vingi haitarajiwi vyama vya upinzani kuminywa kufanya kazi za ubunge bungeni kwa visingizio visivyo na mashiko. Mawaziri kuanza kufanya kazi za uwaziri bila kutangazwa majukumu yao kwenye gazeti la serikai ni jambo la kushangaza. Vyama vya siasa kukatazwa kufanya kazi ya siasa za kidemokrasia huku CCM ikiruhusiwa ni jambo la lishangaza. Watu kuzuiwa kumzika mwananchi aliyeuwa kwa kuvamiwa huku akifanya kazi ya kidemokrasia, hapa namzungumuzia Marehemu Mawazo- RIP. Huyu aliuawa kwa ukatili, polisi wakazuiwa mazishi yake ya heshima na pia viongozi wan chi kushindwa kuonyesha maskitiko kwa mwenyekiti wa CDM mkoa wa Geita kuuawa kinyama ni kati ya mambo yanayozua maswali kama awamu hii ya tano inataka kusimamisha katiba ya nchi kufanya kazi. Tuwakatalie uhuni huu.