Serikali ya magufuli itatenda

Serikali ya magufuli itatenda

jaba jumah

Senior Member
Joined
Sep 24, 2015
Posts
150
Reaction score
50
Usafiri wa Majini
Kwa kushirikiana na sekta binafsi, kuendelea kuboresha huduma za uchukuzi katika
Bandari za mwambao kwa kufanya yatuatayo:-
(a) Kuanza ujenzi wa gati Na. 13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam;
(b) Kukamilisha uboreshaji wa gati Na. 1 – 7 ili kuimarisha utoaji wa huduma katika
Bandari ya Dar es Salaam;
(c) Kuanza ujenzi wa gati la kushusha magari (RoRo) katika Bandari ya Dar es
Salaam;
(d) Kuanza ujenzi wa bandari mpya za Bagamoyo na Mwambani Tanga;
(e) Kuanza na kukamilisha ujenzi wa magati manne (4) ya ziada katika Bandari ya
Mtwara;
(f) Kukamilisha ujenzi wa Bandari ya Nyamisati ili kuboresha usafirishaji wa kwenda
na kutoka Mafia;
(g) Kuendelea kuboresha Bandari ya Mwanza, upanuzi wa Bandari ya Musoma na
ujenzi wa magati ya Ntama, Lushamba na Kiyamkwiki;Kuendelea na uboreshaji wa miundombinu ya bandari za Ziwa Nyasa naTanganyika ili kuimarisha huduma zitolewazo kwa kujenga magati ya Kagunga,Kasanga, Kibirizi, Itungi na Kiwira;(i) Kuboresha mfumo wa uondoshaji mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam kwa
lengo la kuongeza kiwango cha utendaji kwa kuweka mfumo wa “electronic
window System” na kufunga mita za kupima mafuta; na
(j) Kujenga na kukamilisha meli mbili za abiria na mizigo katika Ziwa Tanganyika, meli
moja ya abiria na mizigo katika Ziwa Victoria na meli nyingine ya abiria na mizigo
katika Ziwa Nyasa.
 
Back
Top Bottom