VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,904
Ni vituko,maigizo,mazingaombe na usanii. Hasa kupitia vyombo vya habari. Viongozi,tena waandamizi Serikalini,wanasema wasichofanya na wanafanya wasichosema. Ilimradi,ionekane wanawajibika na kusikika. Wanapenda kushangiliwa kwa wasichokiamini bali wakisemacho.Mazingaombwe na maigizo!
Tanzania imenyimwa mabilioni na kufurushwa na MCC. Wakaibuka viongozi kusema kuwa Tanzania imejiandaa kujitegemea. Ilishajiandaa kukosa fedha za MCC. Wakasema ni muda sasa Tanzania kutotegemea misaada ya nje. Viongozi hao wakapata mashabiki lukuki. Wakashangiliwa kwa kusema ukweli. Mazingaombwe!
Tanzania imepokea msaada wa mabilioni toka Serikali ya Japan. Walewale,wakasifu msaada huo na kusema utasaidia bajeti ijayo. Walewale wakashangiliwa tena na walewale. Za MCC hazitakiwi,za Japan zashangiliwa. Mazingaombwe!
Tanzania bado yahitaji misaada. Bado ina bajeti tegemezi. Viongozi waache kujikaza kisabuni na kuigiza. Waseme ukweli. Waseme kuwa kule Zanzibar demokrasia imekandamizwa. Waseme kuwa sheria ya mitandao ni kandamizi. Waseme kuwa MCC wako sahihi kutunyima fedha zao kwakuwa hatukutimiza masharti. Tujirekebishe ili tupewe. Tajiri hanuniwi!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam