Serikali ya CCM na viongozi wake acha hili kabisa

Serikali ya CCM na viongozi wake acha hili kabisa

daza steven

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2016
Posts
361
Reaction score
361
Kutokana na serikali yetu tukufu ya awamu ya 5 na filosophia yake ya hapa kazi tu nafikiri sasa saa imefika kuacha maigizo katika dhana nzima ya hapa kazi tu.

Naomba kutolea mfano, juzi juzi mkoani Dodoma na mikoa mingine kiongozi mmoja wa juu katika serikali alikuwa akizindua oparesheni ya kupanda miti, ambapo mti mmoja tu ulipandwa.

Zoezi la kupanda kamti kamoja ulikuwa na msafala mkuwa wa magari zaidi ya 40 na viongozi wengi ambao wanalipwa per diemu zao kwa siku kufika pale, hili ni kuharibu kabisa dhana zima ya hapa kazi aliyoanzisha Mh. Dr Joni Pombe Magufuri.

Vinavyosikitisha:
  • Gharama kubwa ya kupanda mti mmoja ni kubwa na hali haliakisi kabisa dhana ya hapa kazi tu na kupoteza pesa nyingi za walipakodi masikini.
  • Kiongozi anayefika kupanda huo mti anakuwa kinyume kabisa na maana ya kazi kwani anatandikiwa zuria jipya kutoka dukani tena la gharama sana hili asichafuke hata kidogo.
  • Pamoja na kukuta shimo hilo limeshachimbwa na kibarua ambaye kalipwa buku 3 tu bado kuna kuwa na mtu wa kumsaidia kufukia shimo vizuri hili kiongozi asichoke na ndoo ya maji ya kunawa baada ya kusaidiwa kufukia shimo hili kwa kiongozi ni aibu hasa katika kipindi hikin cha hapa kazi tu.
  • Waandishi wa habari pia wanakuwa wengi nao wanapotosha kabisa dhana zima ya hapa kazi tu. Maana unakuta waandishi awanasukumana kupata picha ya mtu anafukia kamti kamoja. Hii si habari jirekebisheni waandishi wetu mtawasaidia viongozi wangu.
Naona ipo haja ya kujifunza kupitia picha hizi ili tuwe sirias na tunachokisema na tunachofanya hasa kwa viongozi wangu chama changu cha CCM na serikali yake tukimaanisha kazi tu.

images

Hapa ni kavu kavu tena hatari hata kwa nyoka maana nyasi ni ndefu na zuria hakuna lakini Mzee wetu alikuwa anakamua kazi tu.

securedownload-1.jpeg

Hapa hakuna wapambe wala maji ya kunawa wala zuria wala nyenzo yoyote.

upload_2018-5-27_4-20-26.jpeg


Hapa anapanda miche ya mizazi, mwaka 1964 Tanga alichimba mashimo ma 7 mwanyewe na kupanda kama mfano.

Hili ndilo lilikuwa JEMBE la maono ya hapa kazi tu Baba wa Taifa Julius Kambarage nyerere ambaye mridhi wake ni Dr. JEMBE JONI MAGU.

Hivyo natoa rai yangu kwa viongozi wangu kama hawawezi kupanda hata miti mi6 tu au kuchimba mashimo 6 tu ni bora wakawapa vibarua na waache tabia ya kuweka misafara mikubwa ya magari na garama kubwa za posho za viongozi kwaajiri ya kamti kamoja.

Nawasilisha.
Mzalendo wa kweli
Mzee Daza.
 
Kwanza nawahi siti, pili pamoja na ukweli woote huu hapa hadharani, utashangaa watakuja magamba plus kuja kuupinga. Hivi nyie mmelogwa na nana lakini
 
sasa hivi hatuna viongozi bali tuna watawala wanafiki kupita maelezo,
 
Hata tusiwalaumu hawa wa sasa, wapumbavu no sisi wenywe, tumezoea kudanganywa, wa awamu hii wanakwambia umasikini ni jadi na utamaduni wetu hata wafanye nini hawawezi kuumaliza, bora muwaache wanunue bombardier na ma Airbus kwanza.
Ngoja waje washangiliaji na washereheshaji watuambie kipi kinaendelea, ambacho wengi hatukioni ila wao tu.
 
Wamewazidi mpaka bongo movie kwa maigizo na porojo
 
Back
Top Bottom