Serikali: Tutaendelea kununua VX V8 kwa viongozi wa serikali magari mengine hayafai na hayana ubora

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
FB_IMG_1496841939843.jpg

Serikali imesema matumizi ya magari aina ya Toyota Land Cruiser VX kwa viongozi wake wa ngazi mbalimbali kwa Tanzania Bara yataendelea na haina mpango wa kutumia Toyota Prado kwa sasa kama ilivyo kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Msimamo huo umewekwa wazi leo bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, wakati akijibu swali la mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa aliyehoji ni kwanini serikali isitumie Prado badala ya VX ili kuokoa fedha kutokana na gharama za ununuzi na matengenezo kwa VX kuwa juu kuliko Prado.

Kwa mujibu wa Mwambalaswa, gari moja aina ya VX inanunuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni 220, wakati Prado inanunuliwa kwa shilingi milioni 120 na endapo serikali itanunua magari 200 ya Prado badala ya VX itaweza kuokoa shilingi bilioni 2 ambazo zinaweza kutatua kero ya maji katika jimbo lake la Lupa.
 
Mkuu kuna msemo wa wazaramo "zilongwa mbali zitendwa mbali". Utawala huu wa Mr. Longolongo kauli za kubana matumizi yasiyo ya lazima zimekuwa ndiyo wimbo wa kila siku lakini yanayotendeka sivyo kabisa
 
Hahaha.

Zilongwa mbali, zitendwa mbali. Sakala kandumbwa.

Serikali haijulikani inaenda ama inarudi.

Wananikumbusha machizi wa Solid Ground Family waliimba "Mauza uza, mauza uza mambo zigi zaga ahh, shaghalabaghala".

Mara Pinda aseme serikali itabana matumizi na kutoagiza magari ya fahari. Mara Mbarawa anakwambia bila VX waheshimiwa watafariki wakipanda Prado.

Basi ujinga kila pahala.

Nakumbuka siku moja tumepishana na Mzee Mustapha Nyang'anyi anaendesha Volkswagen Beetle hapo Salender Bridge enzi za Nyerere. Mshua anatoka kanisani kamuona wakapungiana. Akatuambia huyu Waziri wangu.

Nikaona hii nchi kweli tuko sawa. Baba yangu anaendesha gari nzuri kuliko ya Waziri wake na Waziri haoni ajabu.

Leo kupata kazi ya serikali ni tiketi ya kutumbua maisha.
 
Hahaha.

Zilongwa mbali, zitendwa mbali. Sakala kandumbwa.

Serikali haijulikanibinaenda ama inarudi.

Wananikumbusha machizi wa Solid Ground Famiky waliimba "Mauza uza, mauza uza mambo zigi zaga ahh, shaghalabaghala".

Mara Pinda aseme serikali itabana matumizi na kutoagiza magari ya fahari. Mara Mbarawa anakwambia bila VX waheshimiwa watafariki wakipanda Prado.

Basi ujinga kila pahala.

Nakumbuka siku moja tumepishana na kina Mustapha Nyang'anyi anaendesha Volkswagen Beetle hapo Salender Bridge enzi za Nyerere. Mshua anatoka kanisani kamuona wakapungiana. Akatuambia huyu Waziri wangu.

Nikaona hii nchi kweli tuko sawa. Baba yangu anaendesha gari nzuri kuliko ya Waziri wake na Waziri haoni ajabu.

Leo kupata kazi ya serikali ni tiketi ya kutumbua maisha.

Hahahahhahahahahah unamkumbuka JKN,CCM yake ilishajifia siku nyingi hii iliyobaki ya Majangili na Mauaji tu
 
Matumizi wanabana kwenye bunge live

Mnakimbizana na MAKOMBO ya DHAHABU mnaacha DHAHABU inabebwa kilaini,mko busy mnafukuza wabunge kisa MAKOMBO ya dhahabu.

Mkwepa Kodi kwepa tu kodi hakuna namna ,serikali inayosema inapiga vita rushwa na ufisadi inarudia mikataba ile ile y kifisadi aka IPTL.

Inaajiri Mwanasheria aliyeliingizia TAIFA hasara kuwa Waziri kisa homeboy
 
Back
Top Bottom