Serikali tatu haiwezekani

Grand Master Dulla

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2012
Posts
411
Reaction score
152
Katika rasimu hii hii ya katiba mfumo wa serkali 3 hauwezekani na yeyote anayejiona kuwa ni lazima iwepo basi bila shaka anaota na mi binafsi naona ni bora tu angeamka toka katika usingizi wake mana anajipotezea muda wake,hizo njama za kuvunja muungano tumeshazishtukia hazikubaliki.
 
hilo ni jambo liko wazi. Eti marais watatu. Nafuu uvunjike,

ni kero zipi hizo zinafanya mpaka kutengeneza nyazifa za kuwa na ikulu tatu???? It is imposible, tanzania yangu( no utanganyika, no uzanzibar. Let us build our strongest country known as tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 

Kaungane na ma-ma yako uone raha.Sie hili li Muungano hatulitaki.Kama unatulazimisha hebu tuwekee hapa hati ya huo Muungano ndio tutakuelewa.
 
kababu nenda ukale kabab. Mtoa mada na wewe wote ndo mnaoota maana hata hamjatoa suluhisho.
 
Last edited by a moderator:
Serikali mbili ni matatizo! Serikali 3 nazo ni matatizo, sULUHU NI SERIKALI 1 TU...


NAdhani unajua kufikiri vizuri.

Serikali mbili na tatu zote HAZIFAI!! MOJA TU ndiyo serikali

SERIKALI MOJA YA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA


Naomba kuunga hoja yako!!!!!!!!!
 
NAdhani unajua kufikiri vizuri.

Serikali mbili na tatu zote HAZIFAI!! MOJA TU ndiyo serikali

SERIKALI MOJA YA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA


Naomba kuunga hoja yako!!!!!!!!!
Safi sana. Wenye akili timamu wote wanasema kama ulivyosema. Long live tanzania.
 
Kaungane na ma-ma yako uone raha.Sie hili li Muungano hatulitaki.Kama unatulazimisha hebu tuwekee hapa hati ya huo Muungano ndio tutakuelewa.

wewe mzenji wewe mi naona unaota tu serkali ni moja au mbili au hakuna muungano hakuna kinachoitwa serkali 3,wazenj mnaota nyie,wakati british wanaondoka zenji walishamwambia sultan na waziri wake mkuu shamte kuwa zanzbr sehemu iliyokaa haiwezi kuwa nchi mana imekaa sehemu mbaya a wakampa na suluhisho kuwa ni lazima znzbr iingie kwenye shirikisho la EA lakini shamte alikataa,matokeo yake yanajulikana,wanaotaka serkali 3 mara nyingi ni wapemba sasa mi naona ni bora wangejitenga wao,na pemba yao wakatuachia znzbr yetu mana wa unguja wote ni wa-bara kasoro hao wapemba tu na waunguja hawana tatizo na muungano wa serkali 2,wapemba solution yangu wajitenge na pemba yao halafu huku kwetu sisi bara waliowengi si waunguja bali ni wapemba na wao tutawarudisha kwao pemba wakaijenge pemba yao kama wanajiona ni wazalendo sana.
 
Safi sana. Wenye akili timamu wote wanasema kama ulivyosema. Long live tanzania.

Ah vipi wewe bwana hata like hunipi!

Sielewi mjadala ni wanini kuhusu hayo maserikali wakati solution iko wazi. Hata Mwalimu na Karume walilenga serikali MOJA TU!

Watanzania wengi wanapenda serikali moja tu ni akina Shein tu na wenzao wanaoona watakosa ulaji baada ya unguja na pemba kuwa wilaya ama MIKOA!
kUNA KIINI MACHO tu hapa
Serikali moja ndiyo itakayotupeleka NCHI YA AHADI yenye ASALI NA MAZIWA, GESI NA MAFUTA NA KUFUTA UMASKINI
 

wewe ni nani kwenye hii nchi kama sio kidampa. unatoa hoja halafu huonyeshi ushahidi kwanini haiwezekani
 
Mimi napenda kuungana na wazalendo wa kweli wanaotaka Muungano wa serikali moja,kama hamtaki hiyo serikali moja basi tuuvunje muungano kila mtu afate ustarabu wake.
 
serkali 3 ni ndoto mi nashangaa sana baadhi ya wa-bara wenzangu wanashabikia masuala ya srekali 3 bila kufikiria na wanafanya hivyo ili tu kuwaridhisha wa pemba na waarabu bila kujua ni mtego kiasi gani wanajiingiza kwenye pango a simba inabidi tufikirie wa-bara wote tuwe wamoja kwenye suala hili,tukigawanyika bila mantiki ni ahisi sana kuwakatisha tamaa ndugu zetu wa unguja ambao kiuhalisia ni wabara na kuwafanya na wao wabadili mtazamo wao.tusiwe na mawazo kama yale ya warioba ya kutaka kuwaridhisha wa2 wengine wafurahi wakati anajiumiza mwenyewe.
 
Kama umetumwa na mkulu wa magogoni umeula wachuya kijana!

Serikali 3 ndiyo chaguo la watanzania waliowengi wazalendo.

Siyo wewe mwenye maslahi binafsi na serikali mbili.
 
Kilichomsukuma Raisi Kikwete kuanzisha mchakato wa katiba mpya ni kutoka kwa wapinzani, baadhi ya NGOS, wanaharakati, vyombo vya habari na wengineo. Pamoja na kulikubali hili ilikuwa tuanze na kura ya maoni kuwauliza wananchi kama:
1. Wanahitaji muungano au la
2. Wanahitaji muungano wa serikali ngapi? Moja, mbili, tatu ama vinginevyo
3. Utawala utakuwaje.

Baada ya kupata maoni haya ndio angeunda hiyo tume ya kutunga katiba, tume hii ingekuwa tayari inajua inatunga katiba kwa muundo wa serikali ya aina gani sio ilivyo sasa ambapo tume imetunga rasimu ambayo bado ina utata kuhusu muundo wa muungano na ambapo iko katika muelekeo wa serikali tatu ambapo baadhi ya wadau wanapinga.

Utata mwingine uko katika muundo wa bunge la Katiba. Muundo wa bunge ungeundwa kutokana na matakwa ya wananchi kuliko ilivyo sasa ambapo wengi ni wabunge waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambapo hawakuchaguliwa kwa madhumuni haya. Naona uchaguzi ungekuwa kwa madhumuni ya kuunda katiba mpya basi wengi wa hawa waliopo sasa wamekosa sifa na wasingechaguliwa, matokeo yake ndio hawa wanaoongoza katika kudai nyongeza ya posho.

NAUNGA MKONO HOJA YA KUWA NA SERIKALI MOJA. Ingawa hili wenzetu wa Zanzibar hawalitaki kwa kuwa baadhi wana uroho wa madaraka wanaona watatupwa nje ya ulingo wa uongozi. Mpaka sasa maendeleo yaliyopo Zanzibar kama ikiwa ni mkoa basi wao wana maendeleo zaidi ya mikoa yote ya bara, kwa hiyo wako katika advantage kuliko kubaki kama nchi. Believe me or not.
 

Unaota mchana ovyooooo
 
Mimi napenda kuungana na wazalendo wa kweli wanaotaka Muungano wa serikali moja,kama hamtaki hiyo serikali moja basi tuuvunje muungano kila mtu afate ustarabu wake.





:A S thumbs_up:
 
safi sana. Wenye akili timamu wote wanasema kama ulivyosema. Long live tanzania.

mnakubaliana kiuwepesi tu bila kuziwazia changamoto zilizopo?
Hebu muwe muna tafakari kwanza kabla ya kuchangia humu jukwaani!

"serikali 3 ndiyo mkombozi wa kero zote,watanganyika tunataka tanganyika yetu!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…