Serikali shughulikia kero hii ya ving'amuzi

Serikali shughulikia kero hii ya ving'amuzi

Nyamtalakyono

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2015
Posts
795
Reaction score
479
Ndugu zangu na watanzania wenzangu napendwa kutoa masikitiko na kero yangu kwa Serikali kutokana na unyama tunaofanyiwa na makampuni ya ving'amuzi. Kwanza ni pale Kifurushi kinapoisha wanakata local Chanel zote. Pili ni gharama za juu za Vifurushi vyao lakini kibaya zaidi ni tabia yao ambayo ni mbaya ya kupandisha kila mara gharama za vifurushi. Naomba serikali kali isimamie swala hili litafanya watanzania wengi kukosa habari kwa kushindwa gharama wakati ni haki ya kikatiba. TCRA nadhani ni wakati wenu kuwajibika kama EWURA wanavyofanya kwenye mafuta na umeme.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kwa nini makampuni ya ving'amuzi wanakuwa na nguvu hivi.... What's behind the wall??
 
Nadhani kuna ...ubia hapa..

Asante kwa kuliona hili Mkuu, nichague 2020 nikaliseme hadharani.
Sizikwi na pesa Mimi..nataka kuwatumikia watu wangu na kero zinazosolvika kama hizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Azam wanakata hata zile channel zilizovamia (FTA) yaani nafikiria kurudi Star Times maana chaneki iliyonifanya nichukue kisambazi cha Azam wameiondoa.

Vv
 
Kikubwa ndg yangu tafuteni mafundi wa madish wawagungie channels za free to Air maana hii nchi imeuzwa siku mingi. Kuna channel mingi za bure labuda kama ww ni mupenzi wa bongo movie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TCRA WAME LALA WANA SUBIRI KUAMSHWA HUSUSANI HILI SWALA LA KUKATIWA LOCAL CHANNELS
 
TCRA ni kati ya zile agency tatu tz zilizolala fofofofofofoooo, cha ajabu ni hadi pale Rais wetu mpendwa Dr John Pombe Joseph Magufuli atakapomuuliza waziri ama mkurugenzi husika kwamba haridhishwi na utendaji wao, ndio utakapoona mbwembwe na ukurupukaji usio wa nchi hii.

Nb: Rais wetu mpendwa hawezi kufika kila eneo tz ni kubwa sana, sisi watendaji wake tulopewa dhamana tumsaidie kwa kila hali,,,,,,,,,,,,
 
Mimi natumia tv za lg 32" naweka na antena za kawaida, nashika ipp media zote,chanell 10,tv1, star tv ,aljzl, tbc1 ,morning star, yani na nyingine za bure kibao.azam wakafie mbali ligi zao za mpira.hovyo sana hawa jamaa.
 
WaTz mnalialia sana..mnapenda vitu vizuri hela hamna alaf mnaanza kulialia...gharama za uendeshaji zipo juu na vizuri gharama..we unataka uone quality hd videos kwa buku 2..

Mjumbe wa JF kutoka Kiseke- Mwanza
 
Back
Top Bottom