Hashim bin Faustin
Senior Member
- Jan 30, 2017
- 177
- 216
Ndugu wana Jamii, japokuwa baadhi yetu hatumuungi mkono Mh. JPM kwa 100% kwa hatua anazo chukuwa zidi ya baadhi ya watanzania wenzetu. Lakini inabidi ifike wakati tuongee ukweli kabisa katika sakata la Manji na Lema na wengine wote katika Taifa letu. Uonevu si mzuri kabisa , LAKINI HESHIMA NA BUSARA LAZIMA TUWE NAYO.
Tuanze na Manji : Ni Mfanyabiashara tajiri wa Kihindi ambaye utajiri wake umejaa ujanja ujanja , amekuwa tajiri anaye sifika kwa kuwa na mikataba tata aliyoingia na taasisi zetu za fedha na baadhi za kidini na amekuwa analindwa sana na Serikali ya ccm. Amekuwa na jeuri ya hela kupitiliza, pia amekuwa akiwaona wa TZ ni wajinga tu, hana heshima kabisa kwa Jamii zaidi ya kuangalia Maslahi yake binafsi. Hivi juzi baada ya jina lake kutajwa kwenye orodha ya Makonda alilipuka na kuita waandishi wa habari na kushambulia viongozi waserikali na Serikali kwa ujumla kuonyesha kuwa yeye ni mtu safi. Kiukweli alikosa busara/adabu na pesa zake zilimtia kiburi.
Hivyo basi kinachomtokea Manji hivi sasa ni matunda ya Jeuri yake na dharau yake kwa wa TZ na SERIKALI. Na hii ni fundisho kwa matajiri wengine na wananchi kwa ujumla wake kuwa lazima Serikali iheshimiwe hata vitabu vitakatifu vya Dini vimetoa onyo hilo. Hivyo basi Ndugu yetu Manji beba Msalaba wako mambo haya umejitakia Mwenyewe.
Ndugu LEMA : Mh. Lema ni kiongozi wetu na mpiganaji mzuri sana katika kusimamia Maslahi ya wananchi. Lakini jambo moja analikosa huyu Mheshimiwa ni Busara katika uongozi wake pia hana subira kabisa. Kwa kauli ambazo amekuwa akizitoa zidi ya Mh.JPM hazina busara na ni zamauzi kabisa, ni vigumu kuamini kuwa kiongozi kama yeye anaweza kutoa kauli hizo. Kiongozi anatakiwa kuwa kioo kwa Jamii anayo iongoza hivyo lazima awe na Busara iliyo timia katika maisha yake ya kila siku. Utu na Heshima ni jambo Muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Ndugu zangu wengi wetu tuliona na kushuhudia jinsi Mh. Lema alivyo gombana na Mkuu wa mkoa wa Arusha mbele ya umati wa Watu na wageni Wakimataifa kwa hakika tukio lile haikuwa aibu kwa Lema pekeya bali ilikuwa aibu kwa Taifa zima la TZ. Pia tulisikia na kuona jinsi Mh.huyu akimshambulia Mh.Rais JPM katika Bunge kwa Maneno makali na ya kebehi kwa Mkuu wa Nchi kwa kweli alivuka mipaka na anayo yapata hivi sasa ameyapanda Mwenyewe wacha afaidi ukaidi wake na Ushamba pia. Hana wa kumlaumu zaidi ya kujuta na majuto ni mjukuuu.
Masheikh wetu wa ZNZ nao pia wanamakosa yao LAKINI Mh.Rais waonee Huruma hawa ni binadamu wanahitaji Huruma yako kama Mkuu wa Nchi.
Mh.Rais wetu JPM kweli mimi mwananchi wa kawaida naunga mkono juhudi zako sana tena sana , lakini napatwa na wasiwasi/Ukakasi fulani , kama kweli juhudi zako zitakuwa na mafanikio kwa watanzania wote kwa ujumla wake. Kwani naona kama vile Mamlaka inayopo inataka kutengeneza ufalme wake kwa kuondoa vibaraka wa ufalme ulio tangulia. Kwanini nasema hivi. ...!! Taifa lolote lenye nia ya dhati kujikomboa katika umasikini wa Mali na kifikra ni lazima lijijengee utaratibu na sheria Mama zenye nia ya zati ya kukomboa Taifa husika. Hapa kwetu hivi sasa hatuna Katiba imara yenye kuweza kusimamia mambo haya ya uadilifu unayo pigana nayo hivi sasa. Vile vile lazima tuwe na mfumo imara wa Taifa wenye kusimamia Sera zote za uchumi na elimu bila kutegemea utashi wa kisiasa wa Chama fulani au Rais fulani kwa kipindi anachoongoza. Lazima tuwe na utaratibu wa kitaifa wenye kusimamia sera za msingi za taifa letu bila kujali sera za chama au Rais. Tunahitaji katiba ya Warioba ambayo chama chako ccm iliidharau na kuisigina kwa kejeli na matusi huku sisi wananchi wanyonge tukitizama tu kwa uonyonge. Mh. Rais wewe ni binadamu na hujuwi lini Mola wako atakuhitaji mbele ya haki hivyo basi tunaomba hili suala la katiba lipe kipaumbele utupe Tanzania iliyo salama Leo hata hapo Kesho muda wako wa Urais utakapo isha tuweze kuwazibiti hawa mafisadi na wezi wa maliasili zetu kupitia Katiba yetu. Tunaomba sana tena sana turejeshee katiba ya Warioba. Tafadhali tujenge misingi imara ya taifa letu.
Pole Manji ! Pole Lema na wengine pia Hasa Masheikh wetu wa Zanzibar Mola awafanyie wepesi katika kipindi hiki kigumu kwenu na watanzania wote.