masengobangu
Senior Member
- Feb 25, 2014
- 125
- 131
Inaaminika duniani kote vijana ndiyo nguvu ya kupeleka gurudumu la maendeleo mbele kwa nchi husika. Ila kwa serikali yetu imekua tofauti sana, hakuna maneno ya faraja na kutiana moyo kila leo ni kukatishana tamaa.
Mwendazake,aliwahi sema katika moja ya kauli zake kwamba vijana hasa waliozaliwa miaka ya 82, wana tamaa sana, nilistushwa na hii kauli kwa sababu ninachoamini kwa umri wa ujana ndiyo muda wa kuangaika huku na huku kusaka fursa mbalimbali, sasa kwann suala la UTHUBUTU litafsiriwe kama tamaa?
Juzi kati speaker wa bunge anapigilia msumari kwamba sisi vijana si waaminifu,unajiuliza kuna siri gani kati ya vijana na wazee wetu hawa maana kila leo tunatafutiwa majina mabaya tu ya kufanya either tusiaminiwe mahala pa kazi au kufifisha uthubutu wetu juu ya jambo fulani.
Wakati tukitafakari haya mawili, juzi tena limeibuka bungeni kwamba vijana wengi hatuna nguvu za kiume, lengo likiwa lile lile kutubeza,kutukatisha tamaaa na kuahaikisha hatuifikii cake yao kwa hofu.
Swali langu je,nini tufanye au wapi tumekosea kama vijana kwa hawa wazee wetu?