Serikali na CCM acheni kumpa Tundu Lissu umaarufu wa bure!

Inaonekana makada wengi hampendi jinsi Magufuli anavyolishughulikia swala la Lissu...

Hata hivyo nimependa ulivyojenga hoja zako.!
Serikali ni taasisi kubwa sana na haiwezi kuepuka lawama kwa mambo mbali mbali kwa sababu jukumu lake ni kulinda Raia wake.

Kama nilivyosema, serikali kutuhumiwa kutaka kuua au kuua siyo jambo geni kutokana na majukumu yake. Kuanzia serikali ya Mwl. Nyerere mpaka Kikwete zimewahi kutuhumiwa kutaka kuua au kuua.

Ujinga unaojitokeza ni pale baadhi ya viongozi wakuu wa CCM na Serikali wanapoanza kurumbana na Lissu wakati sio wasemaji wa taasisi iliyopewa kisheria jukumu la kiuchunguzi.
 
Kwa kiwango kikubwa ninakubaliana na angalizo lako!
 
 
Umenikumbusha Mwalimu Nyerere alivyowaambia wanaccm kwamba wamwache Mrema abebwe kadri awezavyo.

Na akamshauri Mrema agombee ubunge kwani urais hauwezi, Mrema akabisha na kuamua kugombea urais, matokeo yake kila mtu anayafahamu.
Mrema mpaka sasa hujutia ushauri wa Mwl. Nyerere kwa sababu hakuuchukua.
 

..sidhani kama kukaa kimya ingesaidia.

..hoja za TL ni hoja ambazo hazihitaji muda mrefu kuzipatia majibu.

..nilitegemea uishauri serekali ishirikishe WACHUNGUZI WA KIMATAIFA na itoe taarifa na maendeleo ya uchunguzi kwa wakati.

..pia nilitegemea uishauri serekali imlipie matibabu TL ambaye ni mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni.

..kwa kweli inatia AIBU na INALICHAFUA TAIFA kwamba kiongozi wa bunge la Tz ameshambuliwa kigaidi halafu Bunge na Serekali yake wamekataa kumtibu.

..Again, TL angekuwa hana hoja kama angetibiwa na Bunge, na serekali ingekubali maombi ya familia kwamba wachunguzi toka nje washirikishwe.
 
Hakuna serikali ipendwayo na watu wote duniani na nikosa kusema wasioipenda serikali flan ni wapuuzi, basi na wewe ni mpuuzi kupenda kila serikali ijayo.
 
Mwakilishi wa Wananchi kapigwa Risasi ndani ya makazi ya wabunge na Mawaziri, akitokea Bungeni kuwakilisha wananchi wake alafu unakuja na hoja nyepesi eti CCM na Serikali waache kumpa TL umaarufu..

CCM hao hao kupitia Spika walikataa kugharamia Pesa za Matibabu ,sababu kubwa ilikuwa ni nini kama siyo wahusika wa tukio.

Ni vyema leo TL yupo hai angalau tunaweza kuwafahamu kwa kauli zao,wakiwa majukwaani wanajinasibu nchi ya Amani,alafu Mwakilishi wa Wananchi anapigwa Risasi kadhaa mchana kweupe mpaka leo hakuna Uchunguzi wowote wa kitaalamu uliokwisha fanyika kuhusiana na tukio lile.
Acha waendelee kujianika ubaya wao kwa kumjibu TL, maana nafsi zinawasuta, alafu usijitie sana eti wewe Bonge la mshauri au na wewe unatafuta umarufu humu JF.
 
Leo naona umelala vizuri na akili zako ziko sawa sawia...

Nakubaliana na hili.

Lakini kumbuka kuwa hata hizo taasisi za kiuchunguzi unazotaka ziwe ndizo zinasema zinakaliwa na makada wa CCM haohao!!
Hoja sio ukada bali ni utaalam. Majibu ya kitaalam ni tofauti na majibu ya mtu asiye mtaalam
 
Hoja sio ukada bali ni utaalam. Majibu ya kitaalam ni tofauti na majibu ya mtu asiye mtaalam


Katika mazingira ya utendaji kazi ktk nchi yetu professionally, ni ngumu sana kutenganisha na maslahi yako kisiasa - ukada wa chama...

Na unielewe tafadhali, nasema hivi si kwa sbb currently CCM ndiyo wanatawala....

Bali hata ikitokea leo CHAUMA, Chama Cha Wakulima nk wakashika dola, mkondo wa kiutendaji kwa mfumo wa kiutawala tulionao usiotenganisha dola na chama, utawafuata!!
 
Ujumbe mzuri kama utafuatwa ingawa sijui kama wahusika wataupokea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema vema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya wiki mbili tatu hii issue ya TL itakuwa imefyekelewa mbali..imekufa kifo cha mende
 
Samahani, sielewi vizuri hoja yako.

Naomba unifafanulie zaidi,
 
Umejibu vzr sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…