Serikali mnapowasimishia mishahara watumishi, shida iko kwa nani?

Nasubiri michango ya wadau! Labda nitaelewa alichokiandika mleta uzi 😇
 
Umeandika kwa hasira, sasa tulia, eleza kilichotokea kwa ufasaha, kwa kina, kisha toa maoni. Wewe umeanza na maoni na umesahau habari yenyewe!!
 
ni kweli kuna walimu wa tambaza na Azania nilisikia wamekatiwa mishahara kwa mwez wa pili sasa kisa history sheet haionekani.
history sheet ni ile inayoelezea ur profile km ck ya kuzaliwa, nk.

sasa MTU anakatwa mshahara miezi miwili kisa history sheet. waziri tamisemi ingilia kati
 
wengi sana wanalia juu ya history sheet, KUNA halmshauri ambazo walimu walipeleka taarifa month before, lakin ofisi ya wagurugenzi wa halmashauri husika walipuuzia history sheet. Rafiki angu mmoja anasema, maafisa utumishi wanamalingo sana, wanafanyakazi wakipenda na ndio maana hawajawasilisha taarifa muda unaotakiwa.
 
swala kubwa hapo lilikuwa tabia ya maafisa utumishi kutofanyakazi, inavyoonekana hawajui tangu waajiriwe ama, wao au hata wakuu wa idara zao hawajui nani anatakiwa afanye kazi gani

kwa mfn. kazi ya ku update taarifa sahihi za watumishi ni kazi ya nani na anatakiwa afanye nini

kuhakikisha majina ni sahihi, labda
kuhakikisha watumishi wapya wanaingia kwenye mifumo kwa usahihi
waliokufa kazini
waliostaafu
wanaopaswa kupanda vyeo, waliokwishapanda,
wanaotakiwa kwenda masomoni,
nk
 
Miezi miwili mfululizo, baadhi ya watumishi wa serikali wamejikuta wakiingia hatiani baada ya kunyimwa mishahara yao kwa sababu zisizo na msingi wowote.

Upepo wa Dr Magufuli umewalipua maafsa utumishi na hazina kuwasulubu watumishi wasiostahili adhabu hiyo.

Mwezi Oct watumishi walinyimwa mishahara yao, tukifanya uchunguz tutaona maafsa utumishi hawatimizi wajibu wao.

Ninani anawajibika ku update taarifa za watumishi?

Halmashauri zinamatatizo ktk data zao na kupelekea watumishi wa idara za elimu, afya kilimo kunyimwa mishahara.

Mkoa wa pwani ni wazembe wakubwa katika kuweka taarifa sawasawa.

Hili Jipu linakusubiri mhe. Rais.

ninyi watu wa habar nawashangaa sana habar hii kukosekana, nanyi hamuendani na kasi ya Magufuli?

Nasubiri michango ya wadau! Labda nitaelewa alichokiandika mleta uzi 

mimi pia sijamsoma
Na huyo ndio mtumishi,halafu tunalaumu.
 
Back
Top Bottom