Serikali, Matamko mengi bila ufuatiliaji ni kupoteza muda

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
615
Miezi kadhaa iliyopita kwa mbwembe nyingi kwa macho yangu nilimshuhudia Mkuu wa Mkoa wa Jiji la Dar es Salaam Paul Makonda akiutangazia umma kuwa ameamua kwa dhati kuwaondoa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam, mpaka leo hao ombaomba wapo na wanaendelea na utaratibu wao bila wasiasi wowote.

Lakini kama hilo halitoshi, tulisikia serikali ikitoa onyo kwa wacheza Pool wote kuwa michezo hiyo haitakiwi kufanyika muda wa asubuhi na kuwa vileo vitaanza kuuzwa muda wa jioni, uchunguzi wangu kidogo niliofanya Bar nyingi zinafunguliwa mapema na kuendelea kufanya biashara hiyo bila hofu yeyote.

Amri ya kuwataka wafanya biashara kuhakikisha kuwa wanatumia mashine za EFD katika utoaji risiti kwa kiasi kikubwa limepuuzwa na wapo wafanyabiashara wengi sana ambao hawatoi Risiti hizo. Wanapata ujasiri huo kwa kuwa TRA wameendelea kukaa maofisini bila kuweka mbinu mbadala za kufanya wafanyabiashara watii hilo agizo. Sitaki kubeza ila kwa mtindo huu wa kutoa matamko bila kuwa na mipango madhubuti ya usimamizi na ufuatiliaji ni kupoteza muda
 
Back
Top Bottom