mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 901
- 1,738
Sijajua kama ndio wanatimiza yale yaliyokua yanaimbwa katika ile single ya wataisoma namba au ni kwamba serikali haina pesa.......ukiachilia mbali Wizara kama ya Mali asili na utalii inayonuka madeni kuna Wizara ya Maji na umwagiliaji,kuna wizara ya Ujenzi.Vijana wenu wamejiajiri na mnawakopesha zaidi ya mwaka na wengine unakuta wana mikopo katika taaisisi binafsi ambazo riba yake ni kubwa mno hivi mnafikiria wataendelea kwa hali hii ? Inaumiza sana mnatunganya kua mmekusanya na kilichokusanywa hakionekani na ukweli kwa sasa mnafanya kazi ya kusafisha mauchafu ya JK hapo tunajua bado hamjaanza kufanya kazi yenu ya mhula wa 5 wa uongozi maana jamaa aliacha katafuna nchi kama mchwa....hata hiyo kodi sio ya mhula huu ni malimbikizo ya mhula ulipoita so hatutashangaa makusanyo yakashuka kwa kasi ya mlevi mteremkoni wananchi tunalijua hilo....
Serikali ulichaguliwa na wananchi na hao hao waliokuchagua ndio unataka waisome namba ....mliwavalisha kofia na khanga mkawakusanya kwa malori na matoroli kuwapeleka jangwani leo mnawabomolea nyumba zao na hata wenye vijikampuni mnasaidia kuviua kabisa kwa kutowalipa mnatusubiri miaka 5 tena sijui mtatuimbia single gani safari ijayo.