Serikali legelege.......

Nadhani kitendo cha Ndugai naye kuunga mkono kauli ya Sitta kuwa wapinzani ni wanafiki nahisi kitasababisha wapinzani waanze kutoa kauli za kuudhi kila siku.Badala amuache Sitta ajitetee yeye akaamua kumjibia na kumuunga mkono na akagoma kusikiliza mwongozo toka kwa Halima Mdee.Nadhani hapa CCM wamechokoza nyuki kwani watatupiwa matusi ya kila aina na wapinzani
 
Asante mwananchi!lakini for sure,zipo kauli ndani ya habari hii ambazo zimenukuliwa ndivyo sivyo!mfano!kauli ya kafulila!amesema wabunge wanaruhusiwa na kanununi za ajila yao kutibiwa popote duniani! Sio kwa kutumia mishahara yao. 2. Kauli ya mh Mary nagu,yeye na familia yake wanatibiwa hosp ya wilaya Hanang' na sio anajitahidi kuboresha hosp ya Hanang' 3.kauli ya mh Sita,wapinzani ni wanafiki,mfano swala ya posho,wengine walikuwepo bunge la tisa na walizichukua,leo wanazipinga basi wazirudishe! Nk
 
Mie naongezea Serikali ni legelege na imejaa watu ambao hawastahili kupewa nafasi yoyote ile ya uongozi akiwemo Kikwete, Pinda na wengineo wote ndio maana hadi hii leo wameshindwa kutimiza hata moja ya ahadi zao za 2005 achilia mbali ahadi za 2010, nchi iko kwenye giza, mafisadi bado wanapeta, na wachukuaji bado wanachukua rasilimali zetu ikiwemo dhahabu, misitu, tanzanet, gas n.k. na nchi kutofaidika na rasilimali hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…