GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
- Mnakurupuka kumfungulia Kesi.
- Hamjipangi Kisheria na Kiutetezi.
- Mna Wanasheria ' goi goi ' na wa ' hovyo hovyo ' wasiojua kutafsiri Vifungu Kisheria.
- Mmetanguliza ' Chuki ' za Kisiasa Kwake badala ya kuangalia ' Uhalisia '.
- Mmetawaliwa na ' Mihemko ' wakati mwenzenu katawaliwa na ' Ueledi ' uliotukuka.
- Hamumjui kuliko Yeye anavyowajua ' Kindakindaki '.
- Hamjui kutofautisha kati ya Demokrasia na Siasa za Chama Kimoja.
Na leo narudia tena kusema kuwa kwa jinsi kila siku mnapomkamata na kumfungulia ' Mashitaka ' halafu anawashindeni Mahakama nadhani sasa si vibaya mkawa tu kila siku mnamuamkia ' Shikamoo ' kwani kiukweli anawatoeni ' Jasho ' na ' mnalowa ' hasa.
Nadhani ili kushindana na kumshinda Tundu Lissu Serikali inahitaji kuwa na Wanasheria / Mawakili 10,000 kupambana na Yeye peke yake lakini hawa Mawakili sijui Wanasheria wenu wa Serikali ambao mara kwa mara hupambana nae bado sijaona uwezo wao dhidi ya ' Legal Guru ' huyu Tundu Lissu.
Mwacheni tu Tundu Lissu afanye atakavyo na msimkate tena kwani kiukweli ' mnatuchosha ' sisi ambao mkiwa mnakamata kwa ' mbwembwe ' huko barabarani halafu Yeye anakuja kuwashindeni kiurahisi mno Mahakamani na mnaaibika na mnatuaibisha hata sisi Wana CCM wenzenu.
Najua ukweli huu utawauma ila ndiyo nimeusema hivyo kwani ' mnatuchosha ' na kutunishiana nae kwenu ' Misuli ' halafu hakuna kinachofanyika.
Mnakera!