Serikali kumwaga ajira nchini

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
SERIKALI inatarajia kumwaga ajira kwa askari na walimu katika mwaka ujao wa fedha huku ikisisitiza walimu kwamba watakaokaidi kwenda kuripoti kwenye mikoa ya pembezoni na baadaye kuamua kuomba tena, hawatapewa nafasi kama ambavyo imekuwa ikifanya.

Taarifa juu ya ajira hizo, zilitolewa jana bungeni kwa nyakati tofauti na mawaziri tofauti wenye dhamana na taaluma husika.

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato ya Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2016/17 kuhusu ajira za askari, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alisema wataajiriwa askari wapya 3,700 katika mwaka wa fedha 2016/17.

Kwa upande wa ajira kwa walimu 35,411 wa shule za msingi na sekondari, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jaffo alitoa taarifa hiyo kwenye kipindi cha maswali na majibu.

Ajira polisi Waziri Kitwanga alisema mbali ya kuajiri askari hao, pia watawapandisha vyeo askari 7,140, wakaguzi 1,325 na maofisa 991.

Alisema katika mwaka 2015/16, jumla ya askari polisi wapya 3,882 waliajiriwa, na askari wakaguzi na maofisa 4,065 wa vyeo mbalimbali walipandishwa vyeo kwa kufuata utaratibu wa ajira.

“Aidha, serikali imeendelea kuhuisha viwango vya mishahara na posho mbalimbali, ikiwemo posho ya chakula ambayo iliongezwa kutoka Sh 180,000 hadi kufikia Sh 300,000 kwa mwezi,” alieleza Waziri Kitwanga.

Alisema katika mwaka ujao wa fedha, Jeshi la Polisi litaongeza umakini katika kusimamia nidhamu kwa askari wake kwa kufanya uchambuzi wa kina (vetting) kwa kuchukua vijana waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wanaoomba kujiunga na Jeshi la Polisi ili kuwa na askari wenye nidhamu na moyo wa dhati wa kulitumikia Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa Jeshi la Magereza, alisema linatarajia kutoa mafunzo kwa maofisa na askari 4,975 katika ngazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na yale ya Taaluma ya Urekebishaji.

Alisema ili kukabiliana na changamoto ya uchache wa miundombinu ya makazi kwa askari Polisi, serikali kupitia mkopo kutoka Serikali ya China inakusudia kujenga nyumba 4,136 chini ya usimamizi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi.

Akizungumzia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, alisema jeshi hilo linahitaji vituo 152 Tanzania Bara, lakini kwa sasa lina vituo 57 na kati ya hivyo, 38 vipo katika miji na 19 katika viwanja vya ndege. Alisema huo ni upungufu wa vituo 95 hali inayosababisha maeneo mengi kukosa huduma za zimamoto na uokoaji.

Inategemea kujenga kituo kimoja cha zimamoto na uokoaji katika eneo la Kigamboni katika Jiji la Dar es Salaam na kuendelea na ujenzi wa Jengo la Makao Makuu Tazara - Mchicha, Dar es Salaam.

Aidha, alisema Jeshi la Polisi litaendelea kupambana na makosa yanayovuka mipaka hususani ugaidi, uharamia, biashara ya dawa za kulevya, biashara haramu ya kusafirisha binadamu, wizi wa vyombo vya moto hususani magari, wizi wa kutumia mitandao ya Tehama, bidhaa bandia, na biashara haramu ya silaha na uchafuzi wa mazingira.

Walimu kuajiriwa Kuhusu walimu 35,411 watakaoajiriwa, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Selemani Jaffo alisema uamuzi wa kuwaajiri umetokana na serikali kupokea maombi mengi ya kazi kwa walimu ambao mwaka jana hawakuripoti katika vituo walivyopangiwa pembezoni mwa mji kwa kutegemea kuajiriwa na shule binafsi, lakini hawakufanikiwa.

Jaffo alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF) aliyetaka kufahamu serikali inafanya nini kwa walimu waliopangiwa kwenda mikoa ya pembezoni na Lindi na kwingineko, lakini wakakataa kuripoti.

Alikiri kuwa walimu wengi hawakuripoti katika mikoa ya pembezoni na si Lindi pekee, bali mingine ikiwemo Katavi, Kigoma. Hata hivyo alisema, pamoja na kwamba mwaka huu wanaajiri walimu 35,411 , ambaye hataripoti katika mikoa hiyo na kuishia mijini pekee, hawataajiriwa tena serikalini kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa kuomba tena baada ya kukosa katika shule binafsi.

Awali, Katika swali ya msingi, Mbunge wa Viti Maalumu, LucyMlowe (Chadema) alitaka kufahamu mpango wa serikali uliopo wa kukabiliana na changamoto za uchache wa walimu kwenye shule za msingi na sekondari.

Naibu waziri alisema, ili kuboresha elimu nchini kwa kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani serikali imeendelea kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari.

Chanzo: Habari Leo
 
Huyu waziri Jafo anaonekana muongomuongo maneno meeeengi mpaka mengine anayasahau. Gazeti LA nipashe lilimnikuu akisema walimu elfu 40 binge hili hili wiki iliyopita elfu 40, Jana elfu 35 nadhani siku nyingine akiulkzwa atasema 25000
 
Toka mwaka jana hawajaajiri Waalimu ndio maana wako wengi hivyo .
 
Habari Leo

Ni jambo jema sana. Niombe tu na masilahi yao yazingatiwe kwa wakati.
 
waziri kitwanga mbona majuzi wametoa taarifa kuwa wamesitisha ajira za wizara ya mambo ya ndani???? leo tena wataajiri sijui 3700.
 
Huu sasa upendeleo....inamana watu waliosoma vyuo vikuu kwa fani zingine no ajira.....daaaaah nchi hii

Back
Top Bottom