Wakishamaliza hilo ambalo bila shaka itakuwa ni 2018, wataanza kufanya tathmini kuona ikiwa kila mmoja yupo kwenye grade aliyostahili! Wakimaliza hapo wanahamia kuangalia kuna wanaume wangapi na wanawake wangapi kwenye ajira za serikali!
Wakimaliza hilo watahamia kuangalia wangapi wana degree za UDSM! Wakimaliza hapo wataanza tena kuangalia wangapi wana degree kutoka SUA, Mzumbe n.k... ili mradi tu kupoteza muda!
Kuja kushituka, 2019 hiyoooo... serikali haijaajiri wakati kuna sekta kibao nyeti hazina watumishi!
Hapo watatoa ajira 50,000 halafu watatokea mazuzu kushangilia kwamba serikali imemwaga maelfu ya ajira! Kutokana na uzuzu wao watakuwa wameshasahau kwamba walitakiwa wawe walishaajiriwa miaka kadhaa iliyopita lakini serikali ikafanya janja janja hii na ile ili mradi tu wasiajiri!!!
Poleni ma-jobless mnaotafuta kazi! Anyway, hata mimi ni jobless lakini jobless ambae sipo kwenye msururu wa watafuta ajira.
Ndege kwanza, mengine baadae!
Katika hali ya kawaida hadi sasa serikali ilitakiwa iwe imeaajiri angalau walimu 20K wenye shahada!
UKiweka basic ya 700K, gharama ya walimu 20K ni 14 billion kwa mwezi... 168 Billion kwa mwaka= 336 Billion kwa miaka 2.
Hapo maana yake ni kwamba, pesa ya kununua ndege at your expense bado haijatosha manake hadi miaka 2 ikipita, serikali itakuwa ime-save ONLY TZS 336 billion at the expense of 20K teachers. Hiyo ni pesa kwa ajili ya bombardiers tu bado Boeing!!
So, tunaomba muendelee kuwa "wazalendo!"