Serikali kufanya tathimini ya kazi kwa watumishi wa umma ili kuboresha maslahi

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,316
2,000
Serikali inapitia na kufanya tathimini ya kazi na majukumu ya kila mtumishi wa umma ili kuboresha maslahi ya watumishi wa umma nchini, Kauli hiyo imetolewa na naibu Waziri wa Tamisemi Mh Suleiman Jaffo wakati akijibu maswali ya wabunge kadhaa katika kipindi cha maswali bungeni wabunge walitaka kujua kwann serikali haipandishi madaraja na mishahara kwa watumishi wa umma nchini licha ya zoezi la uhakiki kuisha,
Aidha Mh Jaffo alisema Waziri anaehusika na utumishi wa umma amesema utaratibu wa kupandisha mishahara na madaraja kwa watumishi wa umma upo katika bajeti na watumishi watapewa stahiki zao bila tatizo lolote kwani zoezi la kutafuta wenye vyeti feki na watumishi hewa limekwisha aidha Mh jaffo amesema serikali sasa inapitia na kufanya tathimini za kazi kwa watumishi wote wa umma ili mtumishi apewe anachostahili

TBC live bunge
 
  • Thanks
Reactions: SDG

balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
4,875
2,000
Watumishi wa umma watalipwa zile trillions sijui watu wanaogoka nini?
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
9,990
2,000
Wakishamaliza hilo ambalo bila shaka itakuwa ni 2018, wataanza kufanya tathmini kuona ikiwa kila mmoja yupo kwenye grade aliyostahili! Wakimaliza hapo wanahamia kuangalia kuna wanaume wangapi na wanawake wangapi kwenye ajira za serikali!

Wakimaliza hilo watahamia kuangalia wangapi wana degree za UDSM! Wakimaliza hapo wataanza tena kuangalia wangapi wana degree kutoka SUA, Mzumbe n.k... ili mradi tu kupoteza muda!

Kuja kushituka, 2019 hiyoooo... serikali haijaajiri wakati kuna sekta kibao nyeti hazina watumishi!

Hapo watatoa ajira 50,000 halafu watatokea mazuzu kushangilia kwamba serikali imemwaga maelfu ya ajira! Kutokana na uzuzu wao watakuwa wameshasahau kwamba walitakiwa wawe walishaajiriwa miaka kadhaa iliyopita lakini serikali ikafanya janja janja hii na ile ili mradi tu wasiajiri!!!

Poleni ma-jobless mnaotafuta kazi! Anyway, hata mimi ni jobless lakini jobless ambae sipo kwenye msururu wa watafuta ajira.

Ndege kwanza, mengine baadae!

Katika hali ya kawaida hadi sasa serikali ilitakiwa iwe imeaajiri angalau walimu 20K wenye shahada!

UKiweka basic ya 700K, gharama ya walimu 20K ni 14 billion kwa mwezi... 168 Billion kwa mwaka= 336 Billion kwa miaka 2.

Hapo maana yake ni kwamba, pesa ya kununua ndege at your expense bado haijatosha manake hadi miaka 2 ikipita, serikali itakuwa ime-save ONLY TZS 336 billion at the expense of 20K teachers. Hiyo ni pesa kwa ajili ya bombardiers tu bado Boeing!!

So, tunaomba muendelee kuwa "wazalendo!"
 
linguistics

JF-Expert Member
Jun 22, 2014
4,513

Wazalendo hoyeeeeeeeeee
 
DOnoa

JF-Expert Member
Jan 18, 2017
397
250
Iv hili zoezi la vyet fek lilikua tu upande wa tamisemi zaidi, mbona mashirka ya uma jaman especialy veta mbona hawakutolewa kwenye oroza ya vyet feki, na watu wapo wanajulkana kabsa wanavyet feki, huu ukaguz haukutenda haki
 
mtafiti05

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
963
1,000
Matamko kama haya Jafo ana mwaka sasa anatamka, waziri wa uhakiki nae ana mwaka anahakiki na ktamka tu, hivyo hakna wa kuaminika zaid ya kusubr muda uongee wenyewe hawa viongoz ni porojo tu, wanadanganya watanzania bila hata hofu ya mungu! Subrn July itajurkana ukweli nasio kusikiliza hawa wanasiasa!
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,390
2,000
Nimemsikia eti atawakata juu kwa juu wanaodaiwa na DAWASCO.

Ana sababu gani ya kuwa na Waziri wa Fedha? Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha?

Kila senti tano mpaka aithinishe yeye. Tuna serikali au ufalme?
 
Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
1,179
2,000
Katiya wizara zilizochemka niza Chawene/Jafo,wakifuatiwa na Kairuki mhakiki mkuu wa serikali
 
nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,567
2,000
watumishi wa umma bado wanakumbuka ahadi ya mh. rais aliyotoa may mosi ya promotion, increment na ajira mpya kuanzia july. ukweli ama uwongo wa ahadi ya rais time will tell.
 
SDG

JF-Expert Member
Feb 28, 2017
7,652
2,000
Awam hii ni
Uhakiki----Upembuzi-----Uthibitisho---Tathmini
Inaenda inajirudia,inaenda inajirudia inanenda inajirudia.................wamekuja na masuala ya NIDA na mishahara
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom