Serikali kufanya biashara kutaiathiri Maximalipo na Celcom

Serikali kufanya biashara kutaiathiri Maximalipo na Celcom

Sr. Magdalena

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2011
Posts
803
Reaction score
472
Huu mfumo mpya wa kununua umeme (LUKU) kutoka kwenye makampuni ya simu na miamala kuingia moja kwa moja serikalini bila kupitia MAX MALIPO au CELCOM si jambo jema kwa ustawi wa wafanyabiashara wa ndani na sekta binafsi kwa ujumla, ikumbukwe wateja wakubwa wa kampuni hizi ilikuwa ni serekali kwa miamala kama LUKU, MAJI na MALIPO YA TRA ETC..hii system mpya inakuja kuyauwa haya makampuni, yafikiriwe tafadhari
 
Wabuni vitu vipya..watu tulipie bia bar kwa maxmalipo ..
Max malipo ni kama mtu kati....dalali. Sasa hakuna udalali tena. Ukweli utabaki kwamba hizi biashara zitakufa, watu watakosa ajira. Lakini service kwa watumiaji isiwe comptomised
 
Hamna namna inabidi wafanyabishahra wakubwa Tz wabadilike. Serikali inachukua vyake kwa kasi sana. Sasa hivi biashara itakayolipa ni Ile itakayomfanya mwanachi wa kawaida atoe pesa yake akupe wewe mfanyabiashara. Mara nyingi wananchi wa kawaida mahitaji yao ni ya kawaida sana na yanatatulika kwenye mambo ya kawaida sana. Hapa wafanyabiashara inabidi kuwa wabunifu kweli.
 
Udalali umefika mwisho wake. Unanunua umeme kwa Tigo/M-Pesa hela inaenda Tanesco na fee kwa kampuni ya simu.
 
Udalali kwa vitu virahisi na uwepo wa technologies iliyowazi kwa kila mtu kuitumia ni wizi wa mchana, wabuni world wide products au na wafanyabiashara
 
Back
Top Bottom