Serikali kuanza kuthibiti matumizi ya mitandao ya kijamii maofisini muda wa kazi

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Serikali imeanza mchakato wa kutekeleza mpango wa kudhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii katika ofisi za umma ili kuongeza ufanisi. Mpango huo umelenga kuzuia mitandao ya kijamii ikiwamo Facebook, Twitter, Whatsapp na Instagram.

Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala wa Serikali Mtandao (Ega), Suzan Mshakangoto alisema mpango huo umelenga kuwadhibiti watumishi wa umma wanaotumia mitandao hiyo kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 9.30 alasiri.

Alisema sehemu kubwa ya wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wa taasisi za umma wameshapewa mafunzo mbalimbali kufanikisha mpango huo. Hatua hiyo imekuja baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue kuuagiza wakala huyo miezi mitano iliyopita kutafuta njia madhubuti ya kudhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii ofisini ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

"Mtumishi akishaingia ofisini hataweza kutumia mitandao ya kijamii na huduma za barua pepe nje ya mfumo wa Serikali kama Yahoo na Gmail. Tunawataka watumie mfumo wa barua pepe za Serikali ili wafanye mawasiliano salama," alisema Mshakangoto.

Utekelezaji wa mpango huo huenda ukachukua muda kidogo kuanza kwani Mshakangoto alisema taasisi zote za umma zaidi ya 500 zinatakiwa kuunganishwa kwenye Mkongo wa Taifa lakini huenda ukaanza na taasisi 72 zilizounganishwa zikiwamo wizara zote, wakala wa Serikali na idara kama Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Ega ilianzishwa miaka minne iliyopita kwa ajili ya kujenga mfumo wa mtandao wa Serikali, kuimarisha uratibu, usimamizi na uzingatiaji wa viwango vya Serikali Mtandao katika utoaji wa huduma kwa umma. Pia, kuimarisha mifumo shirikishi ya Tehama na kuboresha uwezo wa taasisi za umma katika kutekeleza Serikali mtandao.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ega, Dk Jabiri Bakari alisema sasa wamejikita kuhakikisha mifumo yote ya taasisi za umma inaingiliana kama ilivyobainishwa kwenye miongozo ya Serikali Mtandao ili kurahisisha mawasiliano na kuongeza uwajibikaji.

Source: Mwananchi
 
Ni sheria ya uumbaji kwamba ili kujua kuna wenye akili ni lazima ujue wajinga ni akina nani na ujinga ni nini, na kujua wachapakazi ni lazima wawepo wazembe pia. Hapa ni kujiaminisha kuwa huko juu serikalini kuna watu ambao ni smart sana wanaoweza kuwadhibiti walio chini yao. Hilo haliko na limeshadhihirika maana katika harakati za JPM udhaifu mkubwa umeonekana kwenye high rank positions kuliko walio chini, walio juu ndio wabadhirifu, wanamdanganya hadi rais na uchafu wote.
Tuachie tu mitandao maana ina positives na negatives na uwezo wa kupick mazuri au mabaya ni ya mtumiaji mwenyewe!
 
Wakitoka maofisini hasira zote za kuchat watamalizia majumbani.

Hakuna kuongeleshana tena.
 
Hii inamaanisha kwamba ukiwa eneo lako la kazi, muda wa kazi na kifaa chako binafsi cha mawasiliano (mfano smart phone) hata hicho kifaa chako kitakatiwa mawasiliano ya whatsapp, facebook, insta n.k. hadi baada ya masaa ya kazi ndiyo mawasiliano yanarudishwa?

Nadhani matumizi ya mitandao hiyo itakayodhibitiwa si yale yanayotokana na vifaa vya mwajiri tu bali hata vya mtu binafsi (mwajiriwa au asiye mwajiriwa) mradi tu awe eneo la kazi na muda wa kazi. Vinginevyo tatizo litakuwa halijapata ufumbuzi wa uhakika.
 
Mkuu mbona unachochea kuni?
 
Mkuu mbona unachochea kuni?
Si kuchochea kuni mkuu. Ila hicho ndicho ninachofikiria kwa sababu naamini wafanyakazi wengi katika kutumia hiyo mitandao ya kijamii wawapo ofisini utumia vifaa vyao binafsi. Katika ofisi ambazo kuna Wi-Fi ndipo wafanyakazi uokoa salio la MB katika simu zao kwa kutumia internet connection ya mwajiri.
 
Hii inamaanisha kwamba ukiwa eneo lako la kazi, muda wa kazi na kifaa chako binafsi cha mawasiliano (mfano smart phone) hata hicho kifaa chako kitakatiwa mawasiliano ya whatsapp, facebook, insta n.k. hadi baada ya masaa ya kazi ndiyo mawasiliano yanarudishwa?

Nadhani matumizi ya mitandao hiyo itakayodhibitiwa si yale yanayotokana na vifaa vya mwajiri tu bali hata vya mtu binafsi (mwajiriwa au asiye mwajiriwa) mradi tu awe eneo la kazi na muda wa kazi. Vinginevyo tatizo litakuwa halijapata ufumbuzi wa uhakika.
. Mbona umeongeza chumvi mpaka wageni waaalikwa wameshindwa kula. jifunze ujue kidogo mambo ya mtandao
 
Si kuchochea kuni mkuu. Ila hicho ndicho ninachofikiria kwa sababu naamini wafanyakazi wengi katika kutumia hiyo mitandao ya kijamii wawapo ofisini utumia vifaa vyao binafsi. Katika ofisi ambazo kuna Wi-Fi ndipo wafanyakazi uokoa salio la MB katika simu zao kwa kutumia internet connection ya mwajiri.
Mkuu Tigo wanatoa Whatsapp na Facebook Bure halafu ndo mbinu bora za mawasiliano ya nje ya nchi sasa itakuwaje wakikataza?
 
. Mbona umeongeza chumvi mpaka wageni waaalikwa wameshindwa kula. jifunze ujue kidogo mambo ya mtandao
Inawezekana kweli nimeongeza chumvi. Lakini kwa vile mimi siyo mtaalamu wa IT ndiyo maana nikaanza post yangu kwa kuuliza swali ili kueleweshwa. Hivyo kama wewe ndugu una uelewa na mambo haya basi tupe darasa ili mimi na wengine tujue kidogo mambo ya mtandao.

Pia mwishoni mwa post yangu nimeonyesha wasiwasi wangu kama angalizo kwamba kama hizo ofisi za serikali zitadhibiti matumizi ya mitandao hiyo ya kijamii kupitia vifaa vya mwajiri tu bila kudhibiti vile vya mtu binafsi (awe mwajiriwa au siyo mwajiriwa) awapo eneo la kazi na muda wa kazi, tatizo litakuwa halijapata ufumbuzi wa uhakika kwa sababu wafanyakazi hao wataendelea kutumia hivyo vifaa vyao binafsi kuchat na kadhalika.

Labda tupate ufafanuzi kwamba hilo la kuzuia vifaa binafsi kupokea mawasiliano ya mitandao hiyo ya kijamii muda wa kazi na katika eneo la kazi kitaalamu haliwezekani. Nadhani umenipata vizuri hoja yangu mkuu.
 
Naunga mkono maamuzi haya kwa asilimia mia. Tatizo la watanzania walio wengi ni wavivu si wafanyaji kazi kwa bidii. Nadhani mfumo wa KPI unapaswa kuanzishwa kwa wafanyakazi wa uma kupima performance zao. Hii ni suluhu kubwa wataacha kutumia muda mwingi wa kazi kuchat.
 
Mfumo wa Key Performance Indicators (KPI) upo serikalini lakini unafanyika kikamilifu kwa taasisi chache tu. Na ukiangalia hata Performance Appraisal kwa kiasi kikubwa ufanyika kiubabaishaji kwa sababu hata wakati wa kuwekeana malengo wasimamizi na walio chini yao wengi hawaelewi vizuri namna ya kutambua KPIs na kuweka malengo yanayotakiwa.
 
Mkuu Tigo wanatoa Whatsapp na Facebook Bure halafu ndo mbinu bora za mawasiliano ya nje ya nchi sasa itakuwaje wakikataza?
Ndiyo maana hata mimi kama layman kwenye masuala ya IT nikajiuliza watu wa IT katika taasisi husika watatumia mbinu zipi ili kuzuia hayo mawasialiano hasa kama mtumishi atatumia device yake binafsi kuperuzi na kudadisi katika hizo Whatsapp, Facebook n.k. Wataalamu watakuja kutufafanulia.
 
Back
Top Bottom