Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,581
SERIKALI wilayani Tunduru katika Mkoa wa Ruvuma imepiga marufuku shughuli zote za jando na unyago kufanyika wakati wa masomo na kuagiza kuanzia sasa shughuli hizo zifanyike wakati wa likizo ili kutoa fursa kwa wanafunzi kuhudhuria masomo yao darasani.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Homera kutokana na wilaya hiyo kuendelea kufanya vibaya kitaaluma na kuwa miongoni mwa wilaya zilizofanya vibaya katika mitihani mbalimbali ya mkoa na taifa licha ya juhudi zake za kuanzisha mikakati ya kumaliza tatizo hilo linaloonekana kuwa sugu wilayani humo.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Homera alisema ni muda mrefu Wilaya ya Tunduru iko nyuma kielimu ikilinganishwa na wilaya nyingine za Mkoa wa Ruvuma huku chanzo kikitajwa ni mwamko mdogo wa elimu kwa wazazi, walezi na jamii mzima ya watu wa wilaya hiyo.
Alisema kwa sasa timu ya viongozi ya Awamu ya Tano ikiongozwa na yeye mwenyewe pamoja na wataalamu wengine wa halmashauri imeweka mikakati kabambe kama vile kuhakikisha shule zote za msingi na sekondari zinatoa chakula cha mchana kwa wanafunzi baada ya kubaini kwamba chanzo cha kufanya vibaya na utoro kwa baadhi ya watoto ni kutopata chakula cha mchana.
Alisema katika mkakati huo, wamejipanga kukomesha tabia ya baadhi ya wanaume watu wazima kufanya mapenzi na watoto wa shule na wengine kudiriki kuoa huku wazazi na walezi wao wakitajwa kuhusika moja kwa moja, kwa kuanza msako wa nyumba hadi nyumba kwa kuwatumia wenyeviti wa vijiji na maofisa watendaji.
Homera alisema mpango wa muda mrefu walionao katika wilaya hiyo ni kuhakikisha kiwango cha taaluma kinapanda ili kuondokana na aibu kubwa wanayopata mwaka hadi mwaka, kwani wanaamini itasaidia kupata wataalamu wengi ambao watakuwa tayari kufanya kazi za utumishi ndani ya wilaya hiyo.
Alisema hakuna sababu ya msingi kwa Wilaya ya Tunduru kuendelea kufanya vibaya kitaaluma kwa kwani ni kati ya wilaya zenye fursa nyingi ambazo kama zikitumika vizuri zitasaidia kuharakisha kukua kwa uchumi kuanzia ngazi ya familia, wilaya na mkoa. Aidha, alisema kukamilika kwa mtandao wa uhakika wa barabara ya lami kutoka Tunduru hadi makao makuu ya mkoa mjini Songea na barabara kutoka Tunduru hadi Dar es Salaam kupitia mikoa jirani ya Lindi na Mtwara ni fursa mojawapo ambayo inaweza kuharakisha maendeleo